Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAKUKURU MKOA WA KAGERA YAWATAHADHARISHA WATIA NIA UCHAGUZI MKUU

Na Lydia Lugakila _ Bukoba


Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoani Kagera imesema haitasita kuwafuatilia na kuwachukulia hatua za kisheria watia nia wote kwa nafasi ya udiwani na ubunge watakaokwenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa na serikali katika kupata uongozi.

Kauli hiyo imetolewa Hajinas Onesphory kaimu mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera  wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2025.

Onesphory amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu tayari Takukuru imeanza kufuatilia watia nia wote ambapo kila siku taasisi hiyo imejiwekea utaratibu wa kuhakikisha  inapata taarifa na kufuatilia.

Amesema kuwa taasisi hiyo ipo imara hivyo itachukua hatua kwa mtia nia yoyote atakayejaribu kukiuka taratibu husika.

"Sisi kama Takukuru tutaangaika na mtia nia atakayekwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali katika kupata uongozi",amesema Onesphory.

Aidha kiongozi huyo amesema kuwa kwa mtu ambaye si mbunge hatoruhusiwa kujihusisha na matukio mbali mbali ya kiharakati ikiwemo michango, kuanzisha ligi za mpira , kutoa misaada kwa watoto yatima pamoja na matukio mengine mengi ya kijamii.

Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya taasisi hiyo ni kuzuia Rushwa ni jukumu lako na langu; tutimize wajibu wetu."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com