Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DIWANI WA SOMANGA AKABIDHI BATI NA KENCHI KWA UKARABATI WA OFISI YA SERIKALI YA KIJIJI CHA SOMANGA SIMU

Diwani wa Somanga Saidi Manjonjo akikabidhi bati na kenchi za Ofisi hiyo ya Serikali ya Kijiji cha Somanga Kilwa Mkoani Lindi
Jengo la ofisi ya Kijiji cha Kata ya Somanga Simu Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi
Diwani wa Somanga Saidi Manjonjo akikabidhi bati na kenchi za Ofisi hiyo ya Serikali ya Kijiji cha Somanga Kilwa Mkoani Lindi
Na Regina Ndumbaro Kilwa-Lindi

Diwani wa Kata ya Somanga, Mheshimiwa Said Manjonjo, amekabidhi bati na Kenchi kwa uongozi wa Kijiji cha Somanga simu kwa ajili ya ukarabati wa paa la ofisi  ya kijiji hicho lililokuwa likivuja. 

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Manjonjo amesema alifahamishwa kuhusu changamoto kupitia katibu wa mafunzo na cccm kata ya somanga nakuchukua hatua ya kufika binafsi kujionea hali halisi kabla ya kuchukua hatua ya kusaidia.

Manjonjo amewahimiza viongozi wa kijiji kuendelea kuwa karibu na wananchi na kufuatilia changamoto zinazojitokeza, ili ziweze kufikishwa kwa viongozi wa juu kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi. 

Amesisitiza kuwa kushughulikia matatizo mapema ni njia bora ya kuboresha huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi katika maendeleo ya kijiji.

Kwa upande wake,mwenezi kata ya somanga ndg said  japhet ametoa shukrani kwa diwani kwa kuweza kuguswa na changamoto hiyo na kuweza kuitatua kwa haraka 

Ameeleza kuwa jengo hilo ni muhimu kwani linahifadhi nyaraka mbalimbali za kiserikali kwani,mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni zimesababisha paa kuvuja, hali iliyovuruga utoaji wa huduma kwa muda. 

Amesema bati na kenchi hizo zitarejesha hali ya utulivu na kuwezesha huduma kuendelea kwa ufanisi.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com