Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani, Askofu Mwombeki amemshukuru Mungu kwa kumuwezesha kupitia kipindi kigumu na hatimaye kupata uhuru wake kupitia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, ametoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign imekuwa mkombozi kwa wafungwa waliokuwa wamefungwa bila hatia.
Kupitia kampeni hiyo, kesi nyingi zimefanyiwa mapitio upya na baadhi ya wafungwa, wakiwemo viongozi wa dini kama yeye, wameachiwa huru.
Tazama video kamili hapo chini Askofu Mwombeki akizungumza baada ya kuachiwa huru
Social Plugin