Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MISA TANZANIA YAPAZA SAUTI KUTETEA MAZINGIRA BORA YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa MISA- TAN Edwin Soko

Na Kadama Malunde _ Malunde 1 blog

Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, wanahabari nchini Tanzania wameendelea kupaza sauti kutetea mazingira bora ya uhuru wa vyombo vya habari.

 Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika – Tawi la Tanzania (MISA TAN) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa sheria rafiki, mafunzo ya mara kwa mara kwa wanahabari, na ulinzi dhidi ya unyanyasaji.

Katika taarifa yao, MISA TAN imeeleza mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika kuboresha sekta ya habari, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari na jitihada za kurekebisha sheria kandamizi. 

Hata hivyo, changamoto kama unyanyasaji, ukamataji holela wa waandishi, na mashambulizi dhidi ya wanahabari bado zimeendelea kudhoofisha uhuru na ufanisi wa vyombo vya habari nchini.

Naye Edwin Soko, Mwenyekiti aliyewasilisha mapendekezo kuhusu hali ya uhuru wa vyombo vya habari, amesisitiza kuwa uhuru wa habari ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote. Alitoa wito kwa serikali kuweka mazingira yanayowezesha wanahabari kutekeleza majukumu yao kwa uhuru, uwazi na uwajibikaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com