Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga umeonesha mshikamano wa kipekee kwa kutembelea vituo vinavyolea watoto yatima na kutoa elimu kuhusu kujikinga na ukatili wa kijinsia.
Wakiwa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society Orphanage Centre, wanachama wa TPF-NET wamekabidhi misaada ya kibinadamu na kuzungumza na walezi kuhusu umuhimu wa kulea watoto kwa weledi na kuwa kinga dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Kaimu Mwenyekiti wa TPF-NET Mkoa wa Shinyanga, SP. Esther Zefania, alisisitiza kwamba kila mmoja anapaswa kuchukua jukumu la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na siyo kuwa chanzo cha vitendo hivyo kwa watoto.
Amesema ni muhimu kwa jamii kuungana na kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa kwa usalama na katika mazingira ya upendo ili kuwaepusha na madhara yoyote.
Huu ni mfano mzuri wa kujitolea na mshikamano katika kuhakikisha kuwa watoto wanaishi katika mazingira bora, na jamii inajitolea zaidi kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
TPF-NET inajivunia kuonyesha kwamba kila mtu ana nafasi ya kuchangia kuboresha maisha ya watoto yatima na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.






Social Plugin