
Waziri wa zamani na Mbunge wa Rorya, Profesa Phelemon Sarungi, amefariki dunia leo jioni katika nyumba yake iliyopo Msasani, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Chifu Sarungi, Martin Sarungi amesema Profesa Sarungi amefariki dunia nyumbani kwake Msasani, leo saa 10 jioni.
Martin amesema Profesa Sarungi siku chache zilizopita alikuwa akisumbuliwa na malaria, lakini alipatiwa matibabu na kupona.
Social Plugin