Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UGENI KUTOKA AFISI YA RAIS ZANZIBAR WAKAMILISHA ZIARA MAALUMU KWA KUTEMBELEA MIRADI MBALIMBALI JIJINI DODOMA



Ugeni kutoka Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji kupitia Taasisi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Zanzibar leo tarehe 06/02/2025 wametembelea Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo "SIDO" pamoja na Soko Kuu la Machinga Jijini Dodoma.

Lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuona namna huduma zinavyotolewa kupitia maeneo hayo na jinsi zinavyowanufaisha mwananchi wa kawaida.

Ziara hiyo imeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi ndugu Condrad Millinga.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com