Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : RC MACHA AZINDUA UGAWAJI WA VYANDARUA MILIONI 1.5 KWA KAYA KUPAMBANA NA MALARIA SHINYANGA

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amezindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya, ambapo vyandarua zaidi ya milioni 1.5 vitagawiwa kwa wananchi katika halmashauri sita za mkoa huo ambazo ni Manispaa ya Kahama, Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Msalala, Ushetu na Kishapu.

Akizungumza leo Jumamosi Februari 8, 2025, wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika katika Kata ya Old Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Macha amewahimiza wananchi kutumia vyandarua vyenye dawa ili kujikinga na ugonjwa wa malaria. 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha

Mhe. Macha amesisitiza kuwa usambazaji wa vyandarua utafanyika kwa usawa, na hakutakuwa na kizuizi kwa wananchi wa maeneo ya vijijini, ambao pia watafikiwa.

 Amewataka wananchi kuachana na imani potofu zinazozungumzia matumizi ya vyandarua, akisema kuwa madai ya vyandarua kupunguza nguvu za kiume au kuleta kunguni si ya kweli.

 "Vyandarua hivi ni salama, vina dawa ya kuulia Mbu, na havihusiani na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, wala kunguni, vitumieni ili mjikinge na ugonjwa wa Malaria,” amesema Macha.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (kulia), akigawa vyandarua.

Aidha amewataka wananchi kuepuka kutumia vyandarua kwa matumizi yasiyokusudiwa kama vile kuvulia samaki, kuzungushia bustani na kufugia kuku na kwamba wanatakiwa wafanye usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuondoa mazalia ya Mbu.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, ametaja takwimu za kiwango cha Maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani humo kwamba ni asilimia 16, huku kitaifa ni asilimia 8.1, na Mkoa huo upo nafasi ya 4 kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Peter Gitanya, naye amesisitiza wananchi juu ya matumizi sahihi ya vyandarua vya serikali na kwamba waachane na imani potofu ili ifikapo 2030 kusiwepo na ugonjwa wa Malaria hapa nchini.

Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji kutoka Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), Victor Sungusia, ambaye ni msambazaji wa vyandarua hivyo, amesema katika Mkoa wa Shinyanga kuna Vituo 600, na watasambaza vyandarua kwa wananchi zaidi ya milioni 1.5 kwa wale ambao walijiandikisha, na zoezi hilo litachukua muda wa siku 10.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamepewa vyandarua hivyo, wameipongeza serikali kwa kuendelea kujali afya zao na kuahidi kuvitumia ili kukabiliana na ugonjwa wa Malaria.

 Vyandarua hivyo vitagawiwa kwa wananchi wa Shinyanga kupitia Wizara ya Afya, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), OR-TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD), na wadau wa afya, kama sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupambana na malaria.

Kila kaya itapokea vyandarua kulingana na idadi ya watu katika kaya hiyo, ambapo chandarua kimoja kitagawiwa kwa watu wawili.

 Usambazaji huu utafanyika kwa wananchi walioshiriki katika zoezi la uandikishaji kaya, ambao walipokea kadi maalum za usajili. Kwa wale waliopoteza kadi zao, watapata vyandarua kwa kwenda katika vituo maalum vilivyohifadhi taarifa za kaya zao.

Zoezi hili ni sehemu ya juhudi za serikali na wadau wake katika kupambana na malaria, ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu hatari katika mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya leo Februari 8,2025 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati akizindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya

Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji Bohari ya Dawa (MSD), Victor Sungusia akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Peter Gitanya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Afisa kutoka OR- TAMISEM Best Yoram akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya Mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (kulia), akigawa vyandarua vinne kwa mwakilishi wa moja ya kaya yenye watu nane  katika kata ya Old Shinyanga wakati wa uzinduzi rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya  

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha (kulia), akigawa vyandarua vinane kwa mwakilishi wa moja ya kaya yenye watu 16  katika kata ya Old Shinyanga wakati wa uzinduzi rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya 

Magari yakiwa tayari kusambaza vyandarua kwa wananchi katika halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga ambazo Manispaa ya Kahama, Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Msalala, Ushetu na Kishapu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, (kulia) wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Wananchi wakifuatilia uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya 

Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga, Saidi Kitinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anold Makombe akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akiagana na wananchi wa Old Shinyanga baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akiwa amembeba mtoto katika kata ya Old Shinyanga baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akifurahia na mtoto katika kata ya Old Shinyanga baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akimpatia zawadi mtoto katika kata ya Old Shinyanga baada ya kuzindua zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa ngazi ya kaya.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com