Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHIFU MAZENGO ATAKA RAIS SAMIA KUENZIWA




Na Dotto Kwilasa ,Dodoma

WATANZANIA wametakiwa kuunga mkono jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kuhifadhi urithi wa watanzani hasa katika kipindi hiki cha utandawazi unaoingiza tamaduni nyingi za kigeni ndani ya nchi ikiwemo lugha, mavazi, vyakula na mwenendo wa maisha.

Hayo yameelezwa Jana Jijini hapa na Chifu Mazengo mtawala wa kimila kutoka katika jamii ya wagogo wakati akizungumza katika Maonesho ya kabila la Wagogo yaliyoshirikikisha wanafunzi wanaosomea masomo ya Urithi wa Utamaduni, Historia na Utalii.

Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo, ufanisi na weledi wa kutoa elimu kwa jamii juu ya kulinda na kuhifadhi urithi wa watanzania.

Chifu Mazengo amesema Rais ameonesha kwa vitendo katika kuhifadhi urithi wa watanzani hasa katika kipindi hiki cha utandawazi unaoingiza tamaduni nyingi za kigeni ndani ya nchi ikiwemo lugha, mavazi, vyakula na mwenendo wa maisha hivyo anatakiwa kuungwa mkono.


Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya mambo ya kale anayeshughulikia maendeleo ya Malikale na Makumbusho, Mwita William amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Malikale itaendelea kushirikiana na chuo kikuu cha Dodoma kwa kushirikiana na Idara ya Historia na Akiolojia ili kuongeza nguvu katika kulinda na kuhifadhi urithi wa Malikale, historia na tamaduni.

Naye, Mkuu wa Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari Chuo Kikuu Dodoma, Dk Deograsia Ndunguru amesema "Lengo la fani hizi katika chuo hiki, ni kuzalisha wataalamu wabobezi watakao hudumu katika kuendeleza na kuhifadhi urithi wetu malikale na kiutamaduni na kutumia rasilimali hizo kama zao la kiutalii ili kushamirisha uchumi wa nchi yetu.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com