
Na Regina Ndumbaro Singida.
Hali hiyo imesababisha baadhi yao kulazwa hospitalini ili kupata matibabu kutokana na majeraha ya kushambuliwa na nyuki hao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwalimu wa shule hiyo, Neema Ng'aa, tukio hilo limetokea ghafla wakati wanafunzi wakiwa darasani wakiendelea na masomo yao ya kawaida.
Kundi la nyuki liliingia shuleni na kuanza kuwashambulia wanafunzi na walimu bila tahadhari yoyote, jambo lililoleta taharuki kubwa miongoni mwa walimu na wanafunzi hao.
Mwalimu Ng'aa ameeleza kwamba hatua za haraka zilichukuliwa ili kuwaokoa waliokuwa wameathirika zaidi, ambapo majeruhi walikimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ya dharura.
Miongoni mwa majeruhi, baadhi wamepata majeraha kutokana na maumivu makali ya nyuki.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dk. Vicent Mashinji, ametembelea shule hiyo baada ya tukio hilo kujionea hali halisi na kuwafariji majeruhi.
Amewahakikishia wanafunzi na walimu kuwa serikali itachukua hatua za kuhakikisha usalama wa shule hiyo unaboreshwa, ikiwemo kupambana na hatari zinazoweza kusababishwa na wanyama au viumbe wengine hatarishi kama nyuki.
Tukio hili limeacha hofu kubwa miongoni mwa wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Sayuni.
Wazazi na walezi wamehimizwa kuchukua tahadhari zaidi ili kuhakikisha usalama wa watoto wao wanapokuwa shuleni, huku mamlaka zikifanya juhudi za kutafuta suluhisho la kudumu kwa tatizo hili.
Social Plugin