AMOS AKAMATWA KWA KUZUSHA BINTI ALIYEFANYIWA UKATILI AMEFARIKI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Amos Lwiza (54) mkazi wa Tegeta Wazo wilaya ya Kinondoni mkoani humo, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mitandaoni kuwa binti mkazi wa Yombo Dovya ambaye video zake zilisambaa mitandaoni akibakwa na kulawitiwa na vijana watano kuwa amekutwa tayari kashafariki dunia.

Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Agosti 7, 2024 na kusema binti huyo anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai hajafa, kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na kwamba uchunguzi wa tukio bado uanendelea.

Aidha Kamanda Muliro amesema wanaendelea na uchunguzi kwa waliohusika kwenye tukio la ubakaji na ulawiti.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post