MBUNGE UMMY AUNGANA NA TAASISI YA SHITTA KUTOA SADAKA WAGONJWA BOMBO HOSPITALI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KUCHINJAMBUNGE wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aungana na Umoja wa Taasisi za Kiislamu Mkoani Tanga (SHITTA) kutoa sadaka kwa wagonjwa waliolazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) kusherehekea sikukuu ya Eid Al_Adha kwa ajili ya kuchinja.

Mbunge Ummy alisema kwamba kushiriki kwa pamoja kutoa chakula kwa wagonjwa, kwenye Hospital hiyo  ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha kutawawezesha wagonjwa nao waweze kufurahia siku hiyo 

Akiwa Hospitalini hapo Mbunge Ummy alionyesha  furaha yake kutambulishwa shirikisho hilo  ambalo linaziunganisha Taasisi za dini ya kiislamu katika mkoa wa Tanga huku akiwatoa wito kwa taasisi nyengine kuona umuhimu wa kutoa sadaka kwa wahitaji ikiwemo wagonjwa.

"Kwa kweli nimefurahi sana kushirikiana na Taasisi hii,wakati mwingine mimi kama mbunge napata shida kuzungumza na taasisi moja moja ,lakini kama nataka kukutana na taasisi za kiislamu naweza kuitafuta SHITTA ambayo inaweza kuniletea taasisi zote",Alisema mbunge wa Jimbo hilo Ummy Mwalimu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post