DAWASA YAANZA USAJILI MAGARI YA MAJISAFI DAR, PWANI


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza rasmi zoezi la siku saba la usajili, uhakiki na utoaji vibali vya uendeshaji wa huduma ya magari binafsi ya usambazaji Majisafi katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kwa lengo la kulinda afya na usalama wa watumiaji wa huduma hiyo.

Zoezi hilo linafanyika katika maeneo ya Mbezi Makonde, Wazo, Mbezi Kibanda cha Mkaa, Mapinga, Kibaha, Mlandizi na Chalinze kwa lengo la kuwatambua na kuwapa vibali vya kutoa huduma ya Maji kwa njia ya Magari kwa Wananchi ambao hawana huduma au miundombinu ya Majisafi ya Mamlaka.

DAWASA inawahimiza Wananchi kutumia magari ya Majisafi yaliyopata uthibitisho kwa kuwekewa stika maalum zinazowaruhusu kusambaza huduma ya Maji ndani ya eneo lake la kihuduma.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post