KATIBU TAWALA MKOA WA KILIMANJARO AFARIKI DUNIA KWA AJALINA WILLIUM PAUL, HAI.

KATIBU Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda amefariki dunia katika ajali ambayo imetokea eneo la Njia panda ya KIA, Wilaya ya Hai, akiwa kwenye ziara Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo na kwamba ajali hiyo imetokea muda wa saa 8 kuelekea saa 9 mchana leo, Juni 18, 2024.

"Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali,"amesema RC Babu
Muda mfupi kabla ya ajali hiyo, alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.


Katika ajali hiyo inadaiwa kuwa, dereva wake naye kafariki duniani.

CHANZO - MATUKIO DAIMA MEDIA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post