AJALI YA LORI LA KOKOTO, COASTER, GUTA, PIKIPIKI NA GARI DOGO YAUA WATU 13 MBEYA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mnamo Juni 05, 2024 saa 7:20 mchana huko katika eneo la Mbembela, Kata ya lyunga Jijini Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya Tunduma, Gari namba T.979 CVV na likiwa na Tela namba T.758 BEU Scania ikiendeshwa na Dereva aliyefahamika kwa jina la Ross Mwaikambo [40] likitokea Shamwengo likiwa limepakia kokoto, aligongana na Gari namba T.167 DLF Toyota Coaster iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kisha kugongana na Gari namba T.120 DER Toyota Harrier iliyokuwa ikiendeshwa na Dokta.Robert Francis Mtungi [48] Mkazi wa Isyesye .

Aidha, Lori hilo liliendelea kugonga Guta namba MC 660 BCR iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kisha kugonga Pikipiki namba MC 889 CKX iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika na kusababisha vifo vya watu kumi na tatu (13) kati yao wanawake 5, wanaume 8 na majeruhi kumi na nane [18] kati yao wanawake 4 na wanaume 14 na uharibifu wa vyombo vya moto.

Majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu na milli ya marehemu imepelekwa Hospitalini hapo kwa hifadhi na kusubiri k utambuliwa. Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa Gari namba T979CVV/T758 BEU kushindwa kulimudu gari kwenye mteremko.

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dereva wa Gari hilo ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiwa chini ya ulinzi kwa mahojiano zaidi.

 Imetolewa na :
Benjamin Kuzaga - SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post