SEKTA YA KILIMO KUONGEZA AJIRA ZENYE STAHA KUPUNGUZA UMASKINI NCHINI

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025, amesema wizara yake  itaendelea kuwezesha upatikanaji wa ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo kupitia utekelezaji wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Building a Better Tommorrow – BBT).

“Wizara itaendelea kutekeleza mradi wa  mashamba makubwa ya Chinangali, Chunya, Singida na Ndogowe kwa kujenga mabwawa na kuchimba visima kwenye mashamba ya BBT jumla ya hekta 186,086. Vilevile, Wizara itaanza kutekeleza mradi wa BBT katika halmashauri 100 zitakazotenga maeneo yenye ukubwa wa hekta 200 kwa kila halmashauri na kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika maeneo hayo,” amesema Mhe. Bashe.


Programu hiyo inatekelezwa kupitia miradi mikuu minne ambayo ni kuwezesha upatikanaji wa ardhi ya kilimo na uanzishaji wa mashamba makubwa ya pamoja (Block farms) na umilikishaji wa ardhi, kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa vijana na wanawake (BBT - Mitaji), kuimarisha Huduma za Ugani (BBT – Ugani) na kuwezesha upatikanaji wa miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima wadogo (BBT – Visima).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post