SEKTA YA KILIMO KUENDELEA KUFANYIWA MAGEUZI MAKUBWA NCHINI

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025 ambapo katika hotuba yake amesema katika mwaka ujao wa fedha, Wizara itaendelea kutekeleza vipaumbele vitano (5) vya mwaka 2023/2024 kwa kukamilisha miradi iliyoanza mwaka 2022/2023, 2023/2024 na kuanza miradi mipya.


Waziri Bashe amesema Wizara inalenga kukuza Sekta ya Kilimo kwa upande wa mazao kufikia asilimia 5 kuchangia asilimia 20 katika Pato la Taifa, kuendelea kuchangia asilimia 100 ya upatikanaji wa chakula na kuongeza mauzo ya mazao nje ya nchi hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 3 ambapo malengo hayo yatafikiwa kwa kutekeleza vipaumbele sita na mikakati 27.


Aidha, Amesema Wizara imeongeza kipaumbele kimoja na hivyo kufanya vipaumbele vya mwaka 2024/2025 kuwa sita (6) vitakavyotekelezwa kupitia mikakati 27.


Mhe Bashe ameainisha vipumbele hivyo ni pamoja na kuongeza tija na uzalishaji (Increase Productivity and Production), kuongeza ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo,kuimarisha usalama wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao nje ya nchi, kuimarisha Maendeleo ya Ushirika pamoja na kuimarisha Matumizi ya Mifumo ya TEHAMA katika Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post