MRADI WA BBT UMETENGENEZA AJIRA 475,025

"Wizara ilipanga  kutengeneza ajira 428,571 kwa mwaka 2023/2024  kupitia mipango na mikakati mbalimbali ikiwemo  Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT). Ili kufikia  malengo hayo, Wizara imeendelea kutekeleza Programu  ya Jenga Kesho iliyo Bora kwa vijana na wanawake  yenye malengo ya kuongeza ajira zenye staha, kuongeza  tija, kubakiza wakulima katika sekta (retention of  farmers) na kupunguza umaskini.  


Ninapenda kulitaarifu  Bunge lako Tukufu kuwa, hadi Aprili, 2024 ajira  475,025 zimezalishwa katika Sekta ya kilimo sawa na  asilimia 110 ya lengo la kuzalisha ajira 428,571 kwa  mwaka 2023/2024.


Baadhi ya miradi na Programu iliyotekelezwa ni Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora  kwa vijana na wanawake, miradi ya umwagiliaji na  miundombinu ya uhifadhi na masoko." - Waziri wa Kilimo @HusseinBashe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post