ABOOD ATOA VIFAA TIBA VYA MILIONI 28 KWA ZAHANATI 5



Na Christina Cosmas, Morogoro

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz  Abood  amegawa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 28 katika zahanati za kwenye Kata tano za Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto ya kukosekana kwa baadhi ya vipimo kwenye Zahanati.

Mbunge Abood anasema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kutaka kuona wananchi wa jimbo hilo wanapata huduma sahihi za kiafya na kuwa na  watanzania wenye afya na kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Hivyo amewataka wataalamu wa Afya kuvitumia vizuri vifaa hivyo kwa kuleta matokeo chanya.

Ziara ya Mbunge huyo na kugawa vifaa tiba imefanyika katika Zahanati ya Mbete na Towero zilipo kata ya Mlimani, Zahanati ya Kibwe Kata ya Boma, Zahanati ya Uwanja wa Taifa iliyopo Kata ya Uwanja wa Taifa, Zahanati ya Konga iliyopo Kata ya Mzinga pamoja na Kituo cha Afya cha Sina kilichopo Kata ya Mafisa.

Vifaa vilivyotolewa kwenye ziara hiyo ni pamoja na Vitanda vya huduma ya kwanza vitatu (3), Vitanda vya kusaidia Kinamama wajawazito kujifungua 3 (Derivery Bed) , Hadubini 4 (Microscope Tube) , Sentrifyugi Mashine 5 pamoja na Mashine maalum ya kumsaidia mgonjwa kupumua haswa Kinamama wajawazito.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post