SHINDANO LA MISS TANGA 2024 LAZINDULIWA RASMI

 



Na Oscar Assenga, TANGA

SHINDANO la Miss Tanga 2024 limezinduliwa rasmi huku Mratibu wa Shindano la Miss Tanga 2024 Victoria Martin akisema suala warembo sio uhuni bali ni fursa ambayo inaweza kuwabadilishia watu maisha yao.

Katika kusisitiza umuhimu wa tasnia ya urembo kwamba sio uhuni alimtolea mfanoaliyewahi kuwa Miss Tanzania Jokati Mwogelo manufaa aliyokuwa nayo kupitia tasnia ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu UVCCM Taifa Bara.

Victoria ambaye aliwahi kuwa Miss Tanga 2007 aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa Shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Tanga Beach Resort Jijini Tanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na usajili wa warembo ambao watawania taji hilo huku akitoa wito kwamba usaili bado unaendelea kujitokeza kushiriki kwenye shindano hilo ambalo mwaka huu ltakuwa la aina yake.

Victoria alisema lengo la kuandaa shindano hilo ni aliona ni muda wa kurudi nyumbani ,kuridisha ari na thamani ya urembo ili kuhamasisha ushiriki kwenye shindano hilo ambalo limesheheni fursa mbalimbali.

“Kupitia urembo watu wanaweza kubadilisha maisha yao kwa mfano wapo watu wengi wamenufaika kupiti huku kama ilivyo kwa Jokate Mwegelo ambayo wa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara lakini wapo wengi wametoka kutokana na tasnia hiyo”Alisema

“Lakini kupitia Miss Tanga tunaweza kubadilisha maisha hivyo ni muhimu wadau kuendelee kuisapoti tasnia hiyo kutokana na kuwa sehemu ya ajira kwa vijana wanaoshiriki kutokana na baadhi yao kupata nafasi katika maeneo mbalimbali ambazo zinawakwamua kiuchumi na hivyo kuchochea maendeleo kwenye jamii zao”Alisema

“Tunaomba tujitokeze kwa wingi kusapoti urembo kwani sio uhuru bali ni ajira tumekuwa tukipigwa bunduki kubwa tukiambiwa kwamba urembo ni uhuni sio sahihi maana asilimia kubwa washiriki wanatokea vyuoni “Alisema Victoria

Aidha Mratibu huyo alisema kwamba warembo ambao wanawania taji hilo wanatarajia kuingia kambini Mei 2 mwaka huu Shindano hilo lilitarajiwa kufanyika Mei 11 mwaka huu katika Hotel ya Tanga Beach Resort Jijini humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post