BYABATO ATOA BIMA ZA AFYA KWA WANANCHI BUKOBA


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato akitoa Bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa kwa baadhi ya wananchi wa kisiwa cha Musira


Na Mariam Kagenda - Bukoba

Watu 140 wasiojiweza katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wanatarajia kupata Bima ya afya ya Jamii iliyoboreshwa ili kuwasaidia kupata huduma za afya kwa urahisi kwenye vituo vya vya afya na zahanati za  serikali watakapokuwa na uhitaji wa huduma hiyo.

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Stephen Byabato amesema hayo wakati akitoa Bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa kwa wananchi 18 wa kisiwa cha Musira kilichopo kata ya Miembeni ambapo mbunge huyo ameungana na wadau mbalimbali pamoja na  wanagroup la Whatsapp la Bukoba mjini mpya kutembelea na kuzungumza na wananchi wa  kisiwa cha Musira .

Mhe Byabato amesema kuwa wananchi waliopata Bima hizo kuanzia leo watakuwa wanatibiwa bure kwenye vituo vya afya vya serikali watakapoenda kupata matibabu  ambapo utaratibu wa kuwapatia wananchi Bima  utaendelea katika kata zote za Manispaa ya Bukoba na kila kata watapatiwa watu 10 wasiojiweza.


Amesema kuwa Bima hizo tayari zimeshalipiwa hivyo kwa ambao wameshapata wakati watakapopata changamoto ya afya waende wakatibiwe

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kisiwa cha Musira waliopata Bima hizo wamesema kuwa walikuwa wanapata changamoto ya kupata huduma za afya kwa wakati kwani wakati mwingine wanakuwa hawana pesa  hivyo Bima hizo zitawasaidi sana.


Kwa upande wake Julieth Richard wakati akisoma Risala iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa mtaa wa Musira amesema kuwa katika mtaa huo yapo mambo mengi ambayo yamefanyika ikiwa ni pamoja na ujenzi wa choo,Boti ya Mv Byabato na majiko ya gesi kwa mama lishe ikiwa ni jitihada za kuwakumbuka wananchi wa kisiwa cha Musira pamoja na utoaji wa Siment kwa ajili ya ujenzi wa msikiti .

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima amesema kuwa wananchi wa Kisiwa cha Musira wanahitaji huduma kama ambavyo wanapata wananchi wa nchi kavu hivyo serikali itaendelea kushirikia na wadau mbalimbali wa maendeleo ili waweze kupata huduma mbalimbali za kijamii wanazostairi ambapo ameishukuru kamati ya maandalizi iliyofanikisha shughuli hiyo kutoka group la Whatsapp la Bukoba mjini mpya kwa kushirkiana na ofisi ya mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini.

Mambo mengine yaliyofanyika katika kisiwa hicho ni pamoja na uzinduzi wa choo,upandaji wa miti,uzinduzi wa Boti ya Mv Byabato pamoja na ngazi za kupandia  na kushuka katika Boti hiyo ambayo itawasaidia wakina mama wajawazito na watoto waliokuwa wanapata shida wakati wa kupanda boti.
Wananchi wa kisiwa cha Musira wakitoa zawadi kwa mbunge ikiwa ni ishara ya Shukurani kwa yale aliyowafanyia
Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Adv Stephen Byabato akipanda mti baada ya kufika kisiwa cha Musira
Baadhi ya wanagroup wa kundi la Bukoba mjini mpya baada ya kufika kisiwa cha Musira
Diwani wa kata ya Miembeni Richard Gaspar Gasper wakati akimpokea mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Adv. Stephen Byabato pamoja na wananchi wengine alioambatana nao kwa ajili ya kuwatembelea wananchi wa kisiwa cha Musira

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post