MANDHARI KUELEKEA MAONYESHO YA WIZARA YA KILIMO BUNGENI DODOMA


Kuelekea Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 itakayosomwa Bungeni jijini Dodoma, Mei 2 na Mei 3, 2024, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Kilimo zilizo chini yake wameandaa maonyesho maalumu yatakayowezesha wananchi mbalimbali wakiwemo waheshimiwa Wabunge kuweza kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara hiyo kupitia taasisi zake.

Maonyesho hayo yaliyoandaliwa kwa lengo la kuongeza chachu kwa wakulima na wananchi kuelewa kwa kina dhana ya kilimo cha kisasa na huduma zinazotolewa na Wizara ya Kilimo katika kufanikisha hilo, yanatarajiwa kuanza kesho, April 29, 2024 na kumalizika Mei 03, 2024 katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post