MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KISASA KUDHIBITI MAJANGA YA MIGODI YA BARRICK NCHINI YAPONGEZWA NA SERIKALI NA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA OSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda katika Banda la Barrick

******

Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi wamepongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na migodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu,North Mara na Buzwagi kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa kudhibiti majanga sambamba na kufikisha elimu ya Afya na Usalama kwa wananchi.

Vifaa hivyo vya kisasa vimevutia viongozi mbalimbali,wananchi na wadau mbalimbali wanaoendelea kutembelea banda la maonesho la migodi hiyo katika maonesho ya Wiki ya Usalama Mahali pa Kazi yanayoendelea katika Viwanja vya NaneNane jijini Arusha.

Akiongea baada ya kutembelea banda la Barrick, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ametoa pongezi kwa Barrick nchini kwa kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia usalama kuanzia kwa wafanyakazi mpaka kwenye jamii sambamba na kuwa na vifaa vya kisasa vya kudhibiti majanga.

Nao wananchi wanaotembea banda hilo kwa nyakati tofauti wameipongeza Barrick kwa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya afya na usalama kwa wananchi kupitia maonesho hayo hususani jinsi ya kupambana na majanga ya moto na uokoaji.

Barrick inayo Kampeni ya 'Journey to Zero' inayolenga kuhakikisha wafanyakazi wote wa kampuni wanakuwa salama wakati wote wanapokuwa kazini hadi wanaporudi nyumbani na kampeni hiyo kwa sasaimevuka mipaka hadi nje ya kampuni kuhakikisha jamii nzima inakuwa salama na ndio maana inaendelea kuendesha mafunzo ya usalama kwa jamii ili kuhakikisha jamii yote inakuwa salama
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda katika Banda la Barrick
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda katika Banda la Barrick

Mwenyekiti wa Bodi ya OSHA, Dk. Adelhem Meru akipatiwa maelezo ya usalama mahali pa kazi wa migodi ya Barrick nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya OSHA, Dk. Adelhem Meru akipatiwa maelezo ya usalama mahali pa kazi wa migodi ya Barrick nchini.
Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Barrick Tanzania wakipatiwa maelezo ya usalama mahali pa kazi unavyotekelezwa na kampuni.
Banda la Barrick katika maonesho hayo
Wageni mbalimbali waliotembelea banda la Barrick Tanzania wakipatiwa maelezo ya usalama mahali pa kazi unavyotekelezwa na kampuni.
Timu ya wafanyakazi wa Barrick wanaotoa elimu ya usalama kwenye maonesho hayo
Wafanyakazi wa Barrick wakishiriki zoezi la kupanda miti katika hospitali ya jiji la Aruska katika kutekeleza kauli mbiu ya maonesho ya OSHA ya mwaka huu ya Athari za mabadiliko ya tabia nchi katika usalama mahali pa kazi

Wafanyakazi wa Barrick wakishiriki zoezi la kugawa vifaa vya kutunza mazingira katika hospitali ya jiji la Aruska katika kutekeleza kauli mbiu ya maonesho ya OSHA ya mwaka huu ya Athari za mabadiliko ya tabia nchi katika usalama mahali pa kazi
Timu ya wataalamu wa mazingira wa Barrick katika majadiliano ya uboreshaji shughuli za Usalama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post