ASKOFU FRANCIS LAURENT BUKOMBE ASIMIKWA KUWA ASKOFU MKUU WA KANISA KATOLIKI LA ORTHODOX TANZANIA

Na Mwandishi wetu _ Malunde 1 blog

Aliyekuwa baba Askofu wa kanisa takatifu katoliki la Orthodox Askofu Dkt. Francis Laurent Bukombe amesimikwa rasmi kuwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo Tanzania.

 

Sherehe hiyo ya kusimikwa Uaskofu imefanyika leo Aprili  27, 2024 imeambatana na uzinduzi wa jengo la kanisa takatifu katoliki la Orthodox lililopo Kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga.

Awali akizungumza wakati wa zoezi hilo Askofu Mkuu wa kanisa katoliki la Orthodox Askofu Mkuu Dkt. George Jamba amemsihi kuendelea kutoa huduma kwa watu wa aina zote bila upendeleo .

"Mimi kama Askofu Mkuu nimekubali Baba Askofu Francis Laulent Bukombe kuwa Askofu wa kanisa hili na leo namtangaza mbele ya umati na waumini wa kanisa katoliki la Orthodox hapa  Tanzania, mtumishi anatolewa katikati ya watu na kurudishwa kwa watu, Yesu Kristo alikuja na akawatawadha wafuasi wake ambao walikuwa na shughuli mbalimbali, Yesu aliwaita wakaitika, wito wa Yesu Kristo hata ukiwa nani ni lazima uitike akikuita", amesema Askofu Mkuu Dkt. George Jamba

"MUNGU ametupatia jukumu la kutoa huduma kwa kila mmoja bila upendeleo wowote hivyo nenda kawatumikie watu wa aina yote, nitakupaka mafuta kichwani pamoja na kukuvalisha mavazi kama ishara ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa kanisa takatifu katoliki la Orthodox Tanzania", ameongeza Askofu Mkuu Dkt. George Jamba.

Akizungumza mara baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa kanisa hilo Baba Askofu Dkt. Francis Laurent Bukombe ameahidi kutumikia vyema nafasi hiyo na kushirikiana na serikali katika kupinga vitendo vya ukatili pamoja na kuinga ndoa za jinsia moja .

"Leo hii nimepokea jukumu hili naahidi kutumikia vyema kama vile MUNGU atakavyoniongoza, nishukuru sana wa wale wote waliojitokeza siku ya leo kushuhudia yale yaliyotendeka katika madhabahu hii, niwaombe tuendelee kushirikiana, mimi kama kiongozi wa kanisa hili  niseme tu tutaendelea kushirikiana na serikali katika kukemea na kutokomeza matukio na vitendo vya ukatili kwenye jamii, ubakaji na ulawiti nitasimama kwa nguvu zangu zote kama Askofu kupinga vitendo hivyo”, amesema Askofu Dkt. Francis Laurent Bukombe.

“Nitapinga ukatili kwa watoto vipigo na udhalilishaji kanisa litaendelea kupinga na kuhakikisha malezi bora kwa watoto na jamii kwa ujumla, lakini pia hatutakuwa tayari kubariki ndoa ya jinsia moja, kanisa letu linapinga kwa nguvu zote ndoa ya jinsia moja kama Askofu sitakubali vitu vya namna hiyo”, ameongeza Askofu Dkt. Francis Laulent Bukombe.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amempongeza Askofu Francis Laurent Bukombe kwa kusimikwa kuwa Askofu wa kanisa hilo.

“Hongera sana kwa mambo makubwa ambayo yametendeka kaika madhabahu hii, matunda uliyoyazaa ni ushuhuda wa watu uliyowaita hapa, mengi ulikumbana nayo lakini leo MUNGU amekuinua na kukuchagua wewe kuongoza kanisa hili, ulipo na imani kwa neno litakuwa”, amesema Mhe. Katambi.

Mbunge wa Viti maalum Shinyanga Mjini Mhe. Christina Mzava akizungumza wakati wa sherehe hiyo.

Zoezi la kusimikwa uaskofu likiendelea.


Muonekano wa Kanisa takatifu katoliki la Orthodox lililopo kata ya Masekelo manisapaa ya Shinyanga. 

Muonekano wa Kanisa takatifu katoliki la Orthodox lililopo kata ya Masekelo manisapaa ya Shinyanga. 

Muonekano wa Kanisa takatifu katoliki la Orthodox lililopo kata ya Masekelo manisapaa ya Shinyanga. 




Baadhi ya waumini waliojitokeza kushuhudia zoezi hilo.





Askofu Mkuu wa kanisa katoliki la Orthodox Askofu Mkuu Dkt. George Jamba akiongoza zoezi la uzinduzi wa kanisa hilo.

Askofu Mkuu wa kanisa katoliki la Orthodox Askofu Mkuu Dkt. George Jamba akiongoza zoezi la uzinduzi wa kanisa hilo.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post