GODON FC MABINGWA RAMADHAN CUP 202R.. MNEC QWIHAYA ATOA NENO

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa MNEC Leonard Mahenda Qwihaya amekuwa Mgeni Rasmi katika Fainali ya Ramadhani cup iliyo hitimishwa jana katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kirumba jijini Mwanza.

Fainali iyoo ilikutanisha Timu Mbili ambazo ni Godon Fc Vs  Mamlaka Fc  ambapo Timu ya Godon Fc imeweza kuibuka na Ushindi wa goli 3 kwa Mamlaka Fc 0 Ivo basi Timu ya Godon Fc ni Mabingwa wa Ramadhani cup 2024

Mnec pia aliongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wa Kata jirani pamoja na Katibu wa UVCCM Mkoa Joshua Ramadhani  MNEC Qwihaya alitumia fursa hiyo kuwataka Vijana kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri. anazozifanya

Qwihaya aliongoza Maandamano ya Amani kutoka Ofisi za CCM Kata ya Kirumba kuelekea uwanja wa Shule ya Msingi Kirumba


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post