NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA DUA YA KUMUOMBEA RAIS SAMIA

 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akihudumia chakula wakati wa Iftari iliyofanyika katika Kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma.

Picha ya pamoja katika Iftari katika Kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma ikiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (Mwenye ushungi wa rangi ya orange).

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akikabidhi zawadi kwa ajili ya sikukuu ya Eid katika Kituo cha kulea watoto yatima na wenye mahitiji maalum cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akila chakula na watoto katika Kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa Iftari katika Kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma.


Na. Mwandishi wetu- Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameongoza dua ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan pia ameungana na Viongozi wa Dini na wananchi kupata Iftar ya pamoja.

Akizungumza mara baada ya dua hiyo iliyofanyika jana Aprili 7, 2024 katika Kituo cha kulea watoto yatima cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma, Mhe. Nderiananga amesema kuwa uamuzi  huo wa kufanya dua ya kumuombea Rais Samia ni kwa sababu ya mambo mengi aliyoyafanya katika sekta  mbalimbali  zikiwemo elimu, maji, afya na miundombinu.

Aidha, Mhe. Nderiananga  amewasihi  Watanzania kuendelea kudumisha  amani na utulivu  ili Taifa liendelee kuwa katika hali ya amani na usalama.

“Tumeamua kufanya dua hii maalum ya kumuombea Mhe. Rais  na viongozi wetu wa Serikali pamoja na wazazi wangu”. Amesema Mhe. Nderiananga

Ameongeza “Tunashukuru sana  uongozi wa kituo hiki kwa dua nzuri kwa watoto na malezi mazuri ya hawa watoto wetu naamini wamejisikia vizuri na kufurahi tulivyowatembelea leo”

Naye,  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewashauri watoto hao wasome  kwa bidii ili kutimiza ndoto zao huku akiwataka kuepuka kujiingiza katika makundi mabaya yatakayosababisha kutotimiza malengo yao.

Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi. Rukia Hamis Abdallah ameeleza kwamba kituo hicho kinachohudumia watoto 120 kilianzishwa kwa  lengo la kujiendeleza kielimu katika maadili mema ya dini, kusaidia watoto pamoja na watu wanaishi katika mazingira magumu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post