WANANCHI WAJICHANGISHA FEDHA KUEPUSHA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU



Na Christina Cosmas, Morogoro

WANANCHI wa mitaa miwili ya kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro wamechukua hatua ya kujichangisha shilingi Mil 2.7 zinazohitajika kununua mabomba na kuzuia utiririshaji hovyo wa maji na kuleta uharibifu wa miundombinu ya maji kwa kuyafikidha hadi mto Ngerengere.

Akipokea shingili 510,000 zilizotolewa na wananchi Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini AbdulAziz Abood amesema huo ni ushirikiano mzuri wanaouonesha wakazi wa mitaa hiyo ya Mafisa na Kihonda Mbuyuni ambao unaleta manufaa ya kata na Jimbo kwa ujumla. 

Mbunge huyo ameahidi kuongeza shilingi Milioni Moja ili kufikia shilingi Milioni 2.7 zinazohitajika ambazo zitakamilika pia pamoja na wananchi kujitolea kwa uchimbaji wa mfreji na kurudishia udongo.

Hata hivyo amewashauri watendaji na madwani wa kata mbalimbali katika Jimbo la Morogoro mjini kutimiza majukumu yao ya kazi  na kuhakikisha wanapunguza changamoto za wananchi na hivyo kuwaletea maendeleo.

Awali Diwani wa kata ya Mafisa Joel Kisome amewahimiza wakazi wa mitaa hiyo kujenga tabia ya kuhudhuria kwenye vikao ili kutoa kero na changamoto zao na hivyo kupiga hatua kubwa kimaendeleo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post