RPC MAGOMI AKABIDHI MATOFALI, PESA KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA POLISI KOLANDOTO

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi akikabidhi matofali na pesa kwa Diwani wa kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mussa Elias kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha polisi katika kata hiyo.

Na Mwandishi wetu  -Malunde 1 Blog 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi amekabidhi matofali mia tano na shilingi 660,000/= kwa ajili ya kununua mifuko 30 ya saruji kwa uongozi wa kata ya Kolandoto kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi katika kata hiyo.

Akikabidhi msaada huo leo Machi 22,2024 kwa uongozi wa kijiji na kata Kamanda Magomi amesema kuwa amekabidhi msaada huo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake aliyoitoa ya kuwaunga mkono wananchi wa kata ya Kolandoto katika ujenzi wa kituo cha polisi.

Aidha kamanda Magomi amewataka viongozi wa kata na vijiji na mitaa katika kata ya Kolandoto kushikamana katika ujenzi wa kituo cha polisi ili kituo hicho kiweze kukamilika kwa wakati hali itakayosaidia kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa wakazi wa kata ya Kolandoto na maeneo jirani.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kolandoto Mussa Elias akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo amempongeza Kamanda Magomi kwa kutoa msaada huo hku akieleza kuwa msaada huo utakuwa chachu kwa wananchi kushikamana ili waweze kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha polisi kwa wakati.

Gari likishusha Matofali yaliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomikwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha polisi katika kata ya Kolandoto.Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi akikabidhi matofali kwa Diwani wa kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mussa Elias kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha polisi katika kata hiyo.Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi Janeth Magomi akikabidhi matofali kwa Diwani wa kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mussa Eliasi kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha polisi katika kata hiyuo.Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi akikabidhi matofali na Pesa kwa Diwani wa kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mussa Elias kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha polisi katika kata hiyo.Diwani wa kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mussa Eliasi akihesabu pesa alizopewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi katika kata hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa viji na kata ya Kolandoto baada ya kabidhi matofali na pesa .Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Janeth Magomi akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa viji na kata ya Kolandoto baada ya kabidhi matofali na pesa .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post