UVCCM DODOMA YAELEZA UIMARA WAKE UNATOKANA NA VIKAO VYA MARA KWA MARA





Na Dotto Kwilasa,DODOMA

KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Dodoma Mjini Isack Ngongi amewasisitiza viongozi wa chama ngazi ya kata kuhakikisha wanafanya vikao ili kukiimarisha chama na jumuiya zake.

Ngongi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa kata ya Kikombo ambapo amesema chama hicho ni imara na kwamba uimara wake unatokana na vikao. 

“Viongozi wa chama ngazi kata kuweni wakali  hakikisheni watendaji  wa jumuiya zote  wanafanya vikao mara kwa mara kwasabau uhai wa CCM ni vikao kama kuna atakaye kaidi basi aandikiwe ripoti ili ipelekwe kweye ngazi za juu,”amesema

Ameongeza kuwa:”Lazima tuhamasishe vikao vifayike pamoja kusoma mapato na matumizi  ili kuondoa sintofahamu kwasababu kila kitu kitakuwa wazi,”

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kikombo Emmanueli Manyono  alisema Rais Dk.Samia ameendelea kutoa fedha za kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilometa 16.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post