DKT. BITEKO AZINDUA RAFIKI DODOMA HOTEL, ATOA MAAGIZO KWA WATENDAJI

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko,akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Rafiki Dodoma Hotel Bw. Fladmiry Mallya,wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi Rafiki Dodoma Hotel hafla iliyofanyika jijini Dodoma.Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel iliyofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Rafiki Dodoma Hotel Bw. Fladmiry Mallya,akielezea malengo na mipango ya uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

SEHEMU ya wageni waalikwa wakimsikiliza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Doto Biteko (hayupo pichani),= wakati wa hafla ya uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel iliyofanyika jijini Dodoma.
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Doto Biteko,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Rafiki Dodoma Hotel iliyofanyika jijini Dodoma.

Na. Alex Sonna-DODOMA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka watendaji wa Serikali kuhakikisha wanailea Sekta binafsi na kila mtu atimize wajibu wake kwenye eneo lake na kuondokana na urasimu.

Dkt. Biteko ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Rafiki Dodoma Hotel New Wing.

Amesema kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.


"Maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, ni lazima sisi viongozi wengine tuhakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo na kuacha kuwamisha Kwa makusudi juhudi hizi za wawekezaji Kwa kuwawekea vikwazo vizivyo na rija yeyote,


Na kuongeza kuwa “kama wewe ni Afisa wa TANESCO uliye na wajibu wa kumuunganishia mfanyabiashara umeme ambao mwisho wa siku ataulipia kwa ajili ya mapato yako, huna sababu ya kumwambia njoo kesho wakati kazi hiyo ungeifanya leo.” amesema Dkt.Biteko


Amesema Watendaji ambao ni warasimu lazima waone aibu kwa kuchelewesha shughuli zinazoijenga nchi.

Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia anataka kuona watanzania wakiwa kwenye daraja la kwanza katika nchi yao na pia waweze kufanya uwekezaji ndani na nje ya nchi bila vikwazo vyovyote.

Aidha amesema bado kuna changamoto ya upungufu wa vitanda kwa wageni wa ndani na nje ya nchi hivyo bado kuna kazi kubwa ya kuwekeza kwenye sekta ya hospitality ambapo amewapongeza wamiliki wa Rafiki hoteli na wawekezaji wengine ambao wanaifanyia kazi changamoto hiyo.

Vilevile, Dkt. Biteko ameipongeza menejimenti ya hoteli hiyo kwa kutekeleza dhana ya nishati safi ya kupikia kutokana na kuweka miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye hoteli husika na kutoa wito kwa wananchi kutoharibu mazingira na kutokukata miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa.

Dkt. Biteko amesisitiza umuhimu Idara na taasisi mbalimbali Serikalini kutumia miundombinu ya uwekezaji Jijini Dodoma ambayo ndio Makao Makuu ya Nchi.

Kutokana na hilo ameagiza Watendaji wa Serikali kuhakikisha kwamba shughuli zinazoweza kufanyika ndani ya Mkoa wa Dodoma zifanyike katika Mkoa husika ili pia kutoa fursa kwa wanachi kupata huduma muda wote pale wanapohitaji huduma za watendaji hao.


Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa suala la uwekezaji halina mipaka Kila mmoja anaruhusiwa kuwekeza Kokote kikubwa ni kuzingatia taratibu za uwekezaji hivyo akatumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine kuwekeza hata katika Jimbo lake la Rombo na maeneo mengine.

"Suala la uwekezaji buana halina ukanda Wala ukabila sisi pale kwetu Rombo tuna mpaka madiwani ambao sio wazawa wa pale ila wamekuja wameaminiwa na wanaongiza vizuri tu hivyo hivyo katika biashara ni vyema kuwekeza popote panapokuwepo na fursa ndio maana Leo ndugu yangu Mallya kaja kuwekeza hapa Dodoma Kwa kujenga hoteli hii ya Kisasa kabisa,"amesema Prof. Mkenda


Pia amempongeza Dkt. Biteko Kwa utayari wake kuwatumikia Wananchi wa kada zote akitambua majukumu mengi aliyonayo ila ameweza kuhudhuria na kuzindua hoteli hiyo jambo ambalo litawatia Moyo wawekezaji wengine kuendelea kuwekeza katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.


Naye Katibu tawala Mkoa wa Dodoma Ndg. Ally Gugu amesema Dodoma bado inahitaji uwekezaji Mkubwa kutokana na kuongezeka kwa Idadi kila siku ya watu wanaingia katika Jiji la Dodoma hivyo uwekezaji wa Hoteli utasaidia kuwaepushia wageni usumbufu wa kutafuta mahali pa kufikia Kwa ajili ya Malazi na kumbi za mikutano.


"Dodoma bado inahitaji uwekezaji Mkubwa sana na tunamshukuru Mwekezeji huyu na tunaendelea kufungua milango Kwa wawekezaji wengine kuona fursa hii ya kuja kuwekeza hapa makao makuu ya nchi," amesema Gugu


Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Rafiki Dodoma Hotel Bw. Fladmiry Mallya, ameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji ambayo yanafanya Watanzania kuendelea kuwekeza kwenye nchi yao na hivyo kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kukuza ajira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post