MBUNGE WA SIMANJIRO OLE SENDEKA ASHAMBULIWA KWA RISASI


Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka inadaiwa amenusurika Kifo baada ya Gari lake kushambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana.

Taarifa mbalimbali zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinaeleza tukio hilo  limetokea eneo la Ndaleta, wilayani Kiteto wakati Ole Sendeka akiwa na dereva wake akielekea jimboni kwake Simanjiro.

Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kupitia Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mwakatundu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo amesema limetokea majira ya jioni leo Ijumaa Machi 29, 2024 na washambuliaji wakitokomea.

Endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post