SERIKALI KURATIBU UTEKELEZAJI WA MPANGO WA TAIFA WA DHARURA WA KUKABILIANA NA MADHARA YA EL NINO


Na Mwandishi wetu- Dodoma

Serikali kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu inaendelea kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kuzuia na Kukabiliana na Madhara ya El Nino kuanzia  Septemba 2023 hadi Juni 2024.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa  Idara ya Menejimenti ya Maafa-Ofisi ya Waziri Mkuu (SBU)  Brigedia Hosea Ndagala katika Kikao Kazi cha kujadili utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kuzuia na Kukabiliana na Madhara ya El Nino Septemba 2023 hadi Juni 2024 ambapo alisema  kutokea kwa maafa husababisha madhara ambayo huathiri  utendaji kazi, kuzorotesha maendeleo na ukuaji wa kiuchumi kwa wananchi  na kupotea kwa mafanikio yaliyopatikana kwa muda mrefu na hivyo, kuzorotesha hatua za maendeleo. 

Alisema Maafa hayo yamekuwa yakisabibisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo, ulemavu wa kudumu, upotevu na uharibifu wa mali na miundombinu, na ongezeko la tegemezi kutokana na Watoto kupoteza wazazi.

“Nchi yetu imekuwa ikishuhudia matukio ya majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa na kuathiri mfumo wa kawaida wa maisha ya jamii. Maafa haya yamekuwa yakisabibisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo, ulemavu wa kudumu, upotevu na uharibifu wa mali na miundombinu,”Alisema Brigedia huyo.

Aidha Brigedia Ndagala alizitaka kila  sekta kuwasilisha  tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kuzuia na Kukabiliana na Madhara ya El Nino ambao una lengo la kuhakikisha serikali na wadau wanachukua hatua stahiki kuzuia au kupunguza madhara na kujiandaa kukabili na kurejesha hali kutokana na maafa yanayosababishwa na El Nino ili kuokoa maisha na mali.

“Hatua hii ni muhimu ili kuweka mikakati ya pamoja kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa mvua za Masika. Ni imani yangu kuwa kikao kazi hiki kitatoka na mikakati madhubuti itakayosaidia kuendelea kuongeza ufanisi katika kukabiliana na maafa,” Alieleza.

Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Brigedi Hosea Ndagala akizungumza wakati akifungua  Kikao Kazi Cha Kujadili Utekelezaji Wa Mpango Wa Taifa Wa Dharura wa Kuzuia na Kukabiliana na  madhara ya mvua za El Nino  kikao kilichofanyika  Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Luteni Kanali Selestine Masalamado akichangia wakati wa wasilisho la Madhara yaliyotokana na mvua za El-Nino katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Udhibiti na Usimamizi wa Ubora wa huduma za hali ya hewa  kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. Geofrid Chikojo akitoa wasilisho kuhusu taarifa ya muelekeo wa mvua za msimu wa masika kwa mwezi Machi hadi Mei 2024 katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Dodoma. 

Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Morogoro Ndug. Anza-Amen Ndossa akichangia mada wakati wa wasilisho lililohusu madhara yaliyotokana na mvua za El-Nino  katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Dodoma      .

Picha ya pamoja ya washiriki wa kikao kazi cha Kujadili Utekelezaji Wa Mpango Wa Taifa Wa Dharura wa Kuzuia na Kukabiliana na madhara ya mvua za El Nino katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post