RAIS SAMIA MBEBA MAONO WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA




Na Dotto Kwilasa, Dodomaa. 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amewaahidi watanzania kuibeba ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa kutafuta fedha zaidi kukuza nishati ili kuitunza misitu na kuhifadhi mazingira . 

Dk. Samia amezungumza hayo kwa njia ya simu leo Machi 9,2024 wakati Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililonyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma lenye lengo la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikianch na kuhamasisha matumizi ya nishati safi kukabiliana na manadliko ya tabia nchi. 

Amesema, "Nimeibeba ajenda ya Nishati Safi ya kupikia hapa nchini, nitatafuta fedha kwa ajili ya kukuza matumizi ya nishati safi yakupikia kwa ajili ya wanawake, agenda hii  nitaibeba kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu wa Rais na Wizzara ya nishati, " Amesema

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema mwathirika mkubwa wa athari zitokanazo na matumizi ya nishati chafu ya kupikia ni mwanamke hivyo kuna haja ya kupunguza gharama ya gesi.

Aidha ameongeza kuwa athari hizo huchangia magonjwa yanayopelekea vifo takribani 33,000 vya watanzania kila mwaka, ambapo asilimia kubwa ya vifo hivyo ni kina mama na watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambao hutumia muda mwingi jikoni na mama zao . 

Naye Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk.Dotto Biteko amezitaka kampuni zinazojihusisha na uzalishaji wa mitungi ya gesi ya kupikia kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.

Amesema kampeni ya nishati safi ya kupikia ni ya nchi nzima na safari yake ilianzishwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan baada ya kuzindua mpango wa nishati safi ya kupikia kwa wanawake wa Afrika akiwa katika mkutano wa kidunia.

Aidha amewaomba viongozi wa Serikali pamoja na taasisi kuelewa kwamba ajenda ya nishati safi sio ya Serikali peke yake bali ni ajenda ya wote, hivyo waisukume kuhakikisha mwanamke wa Tanzania anapata hadhi

Dk. Biteko pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba wanaume wote nchini kujipa wajibu wa kutimiza majukumu yao kwenye familia ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kuwezesha wanawake kupika kwa urahisi na kuokoa afya zao kutokana na moshi wa kuni. 

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema kuwa kuanzia Julai mwaka 2021Wizara hiyo imekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali yaliyotolewa na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa ifikapo mwaka 2023 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Amesema pia hatua ya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa nishati safi ya kupikia kugawa majiko ya gesi pamoja na majiko banifu ni muendelezo wa juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha ifikapo mwaka 2033 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Oryx Gas Benoite Araman amesema kupika kwa gesi ya Oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti huku akisisitiza zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa.

Amesema wanawake wanatumia muda mchache kupika hivyo wanapata nafasi kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuepuka kugombana na wenza wao kwa kuchelewesha chakula, na wanaume pia watajiongezea marks ukiwazadia wamama mitungi ya gesi.Kwa kutumia gesi ya Oryx, Watoto wanakua na muda mwingi zaidi kusoma na sio kwenda kutafuta kuni. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post