UWT WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWATUA KUNI KICHWANI

 




Na Dotto Kwilasa,Malunde Blog 1,DODOMA.


MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan kwa maono yake juu ya kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya Nishati safi ya kupikia na kueleza kuwa jambo hilo  litawezesha kuwatua wanawake kichwan kuni na kuwapa nafasi ya kujiinua kiuchumi.
Mwenyekiti huyo ameyasema hayo leo Machi 9 , 2024 kwenye kongamano la wanawake la ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia jijini Dodoma,ambapo amesema sasa wanawake wanakwenda kuachana na Matumizi ya kuni na mkaa hali itakayopelekea utunzaji wa mazingira katika jamii. 

Akizungumza kwenye kongamano hilo Chatanda ameiomba Serikali kupunguza bei ya Nishati ya gesi ili wanawake Waweze kuachana na Matumizi ya kuni na mkaa kwenye shughuli za mapishi.

" Bei ya Nishati safi ya Gesi ya kupikia ikipungua tofauti na ilivyo kwa sasa basi wananchi wengi wakiwemo wanawake wataweza kununua majiko na kuachana na Matumizi hatarishi ya kuni,bei ikipunguzwa madukani wanawake watakuwa na uwezo wa kununua kila inapoisha,"amesema 

Aidha amewapongeza waandaaji wa kongamano hilo ambao ni wizara ya Nishati kwa kuwaalika wanawake zaidi ya 10,000 kutoka mikoa tofauti tofauti na kuwapatia elimu na vitendea kazi vya nishati. 

Amesema kupitia mfuko wa Nishati umesaidia kuboresha huduma za nishati kwa gharama zenye ubora kwa watu wa chini na kuiomba Serikali kuona namna ya kuwezesha gesi ya majumbai kupatikana kwa gharama nafuu na kuwezesha majiko yanayotolewa kutumika kama ilivyokusudiwa. 

'Tumeona Serikali ikipambana na utunzaji mazingira na kutenga Baheti ya nishati safi ya kupikia kwa mwaka wa fedha 2024,hatua hii itasukuma wanawake kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa na kulinda mazingira na afya na kuwa na muda wa kutosha kufanya shughuli za uzalishaji mali,"amesisitiza na kuongeza;

Sisi wanawake tunakwenda kuwa wadau wa mazingira kupitia nishati safi ya kupikia na kuwezesha wanawake wengine kuacha kutumia kuni ili kulinda uhifadhi wa mazingira"amesema



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post