NEMC YASHIRIKI ZOEZI LA UPANDAJI MITA 300 KUMUENZI WANGARI MAATHAI

 Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akipanda mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA  la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  (NEMC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Kenya Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) pamoja na wadau mbalimbali wameshiriki katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani.

Hafla hiyo ya upandaji Miti kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai imekuwa ikiadhimishwa Machi 3, kila mwaka.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Machi 16, 2024, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mary Maganga, amesema mti ni mmoja ya kiungo cha dunia kinachoiwezesha kuishi kwani inaleta hewa, mvua, chakula na kulinda ardhi.

“Hivyo, siku ya leo tunaisherehekea hii siku kama Afrika ikiwamo Tanzania kwa mchango mkubwa wa Kenya ambayo inasimamia Jumuiya ya Kimataifa inayoshughulikia mazingira, pia tunamsherehekea Mama Wangari ambaye alikuwa kinara Tanzania kutokea Kenya katika nyanja ya utunzaji wa mazingira na alikuwa kinara katika upandaji miti kwa mtu mmoja mmoja ndani ya Bara letu la Afrika na ni mwanamke wa kwanza kupewa tuzo ya Nobel rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa.

“Kama Afrika na familia ya Afrika lazima tuwe kinara kuhakikisha kwamba mazingira yetu yako safi, yako hai na tunashughulikia hali ya mabadiliko ya tabianchi, tunadhibiti hatari yakutokea kwa jangwa, hivyo hali hii ikiendelea hivi ilivyo hivi sasa tutashindwa kuishi sababu mti ni uhai,”. Amesema Dkt. Immaculata.

Kwa upande wake Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga amesema kila mmoja analo deni na jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba anatunza mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema mazingira ambayo tunajivunia hii hivi sasa ni sababu ya kuwapo kwa watangulizi ambao walijitoa kwa kupanda miti na kuitunza na leo inasaidia kuzalisha chakula, maji na mahitaji mengine.

“Katika mambo ambayo Wangari alihimiza na kuzingatia ni kwamba sisi tuna wajibu kama kizazi kilichopo sasa kupanda mti ili kukisaidia ama kutunza mazingira na hali ya maisha ya vizazi vijavyo.

“Hivyo, kila mmoja wetu ana jukumu na deni la vizazi vijavyo katika utunzi wa mazingira, kwani haya tunayojivunia sasahivi ni sababu kulikuwa na watu waliopanda miti na kuitunza na ndiyo sasahivi tunapata maji, hali ya hewa nzuri na chakula, hiyo ndiyo sababu inayotukutanisha katika siku yake na kuzingatia mambo aliyoyatilia mkazo siyo Kenya peke yake bali Afrika na Duniani kwa ujumla,”. Amesema Balozi Njenga.

Akihitimisha hafla hiyo iliyoambatana na zoezi la upandaji miti , Naibu Kamishna Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania Bi.Carolen Mavunde kwa niaba ya Kamishna wa hifadhi  wa  wakala wa huduma za misitu Tanzania amesema msitu huu unaukubwa wa hekta 8965, unaaina 80 za ndege na 14 za wanyama wadogo pamoja na mimea ambayo Iko hatarini kutoweka.

 Aidha amesema kuwa miti iliyopandwa katika hifadhi hiyo ni ile inayostahimili ukame huku akiitaja baadhi yake kuwa ni migunga na mkangazi ambayo huoteshwa kando ya mto.

Hata hivyo kwa mwaka huu sherehe hizo zilisogezwa mbele baada ya kifo cha Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia Februari 29, 2024.

 Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akiwa na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga, Naibu Kamishna Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania Bi.Carolen Mavunde pamoja na wadau wengine mbalimbali wa mazingira wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshika mche mmoja wa mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.
 Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akiwa na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga, Naibu Kamishna Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania Bi.Carolen Mavunde pamoja na wadau wengine mbalimbali wa mazingira wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshika mche mmoja wa mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.
 Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akipanda mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.
 Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akipanda mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.
 Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akipanda mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga akipanda mti katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga akizungumza katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akizungumza katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

 Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi akiwa na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Balozi Isaac Njenga, Naibu Kamishna Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania Bi.Carolen Mavunde pamoja na wadau wengine mbalimbali wa mazingira wakiwa kwenye picha ya pamoja katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.
Wadau mbalimbali wa mazingira wakiwa kwenye katika zoezi la upandaji miti 300 kwa heshima ya Mazingira ya Afrika na Siku ya Wangari Maathai katika Hifadhi ya Mazingira ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani leo Machi 16, 2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments