MIKATABA 56 YASAINIWA KWA AJILI YA MATENGENEZO YA BARABARA MKOANI MARA

Wakandarasi wa barabara mkoani Mara wamesaini mikataba 56 yenye thamani ya shilingi Bilioni 14.5 kwa ajili ya matengenezo ya barabara maeneo ya mjini na vijijini.

Akiongea na waandishi wa Habari Meneja wa wakala wa Barabara za Vijijii na Mjini TARURA Mhandisi, Mwita Charles amewataka wakandarasi hao kuanza kazi mapema ili waweze kumaliza kazi kwa wakati.

“Tumesaini mikataba 56 ya shilingi bilioni 14.5 na kila Halmashauri ina kiwango chake cha fedha, mfano tuna kilometa za kawaida zaidi ya 160, mitaro zaidi ya kilometa 8 na taa za barabarani 145 kwa miji yetu, Musoma, Rorya, Bunda na Tarime” , alisema Meneja TARURA Mara.

Kwa upande wa Wakandarasi hao wameahidi kufanya kazi kwa muda ulipangwa ili kuweza kuondoa kero na changamoto zilizopo sasa kwenye baadhi ya barabara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post