JENGO JIPYA LA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA LAFUNGULIWA SHINYANGA


Muonekano sehemu ya jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga - Picha na Mpiga Picha Wetu Malunde 1 blog
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akikata utepe ikiwa ni sehemu ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa.

Na Mapuli Kitina Misalaba - Shinyanga

Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu amefungua rasmi jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa.

Hafla ya ufunguzi wa jengo hilo  imefanyika leo Machi 16,2024 katika viwanja vya jengo hilo lililopo katika eneo la mtaa wa Miti Mirefu Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali  kutoka nje na ndani ya Mkoa wa Shinyanga.

Katika taarifa yake Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini ,Sylivester Mwakitalu amesema majengo mengine ya mashtaka yapo katika Mkoa Mikoa ya Mbeya, Katavi, Rukwa, Pwani, Ilala, Morogoro, Geita, Manyara pamoja na Njombe.

Amesema ili watumishi waweze kutoa huduma bora kwa wananchi ni muhimu kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watumishi ikiwemo kujenga ofisi zenye majengo bora na vitendea kazi katika Mikoa na Wilaya zake.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kutokana na kukamilika kwa majengo hayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yaliyokusudiwa katika utoaji wa huduma bora hasa kwenye eneo la haki jinai.
“Muundo wa ofisi ya Taifa ya mashtaka unaelekeza kuwepo kwa ofisi za mashtaka Mikoa na Wilaya zote, hadi sasa zipo ofisi za mashtaka katika Mikoa yote ya kiserikali pamoja na Mikoa minne ya kimashtaka hivyo kufanya jumla ya ofisi za Mikoa Thelathini (30) na zote zinafanya kazi”,amesema.

“Katika utekelezaji wa miradi hii mtaalamu mwelekezi ni chuo cha Dar es Salaam kwa miradi kumi ya ofisi za Mikoa kwa thamani ya Shilingi 1,799,000,000 na wakala wa majengo Tanzania kwa mradi wa ujenzi wa ofisi ya Taifa ya mashtaka makao makuu kwa gharama ya Shilingi 1,845,000,000”,amesema Sylivester

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu amesema ni vema kila mmoja kuhakikisha anatekeleza majukumu ya ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa mujibu wa wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali iliyopo.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuleta maboresho makubwa katika mnyororo wa utoaji wa huduma ya haki jinai huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushinikiza suala la haki jinai.

“Ni matarajio yangu uthubutu wa ofisi katika miradi ya ujenzi kama hii na mambo mengine utaendelezwa na hivyo kuleta maboresho makubwa katika mnyororo wa utoaji wa huduma ya haki jinai kwa kusogeza huduma karibu na wananchi na hatimaye kupata haki kwa wakati”,amesema.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu.

“Sote ni mashahidi kwa kuona na kusikia Rais Samia Suluhu Hassan anavyotilia mkazo suala la haki jinai ikiwemo kuunda tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi ya haki jinai napenda nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia yake ya dhati ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta hii ya haki jinai”,amesema Dkt. Kazungu.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga (inayojumuisha mikoa ya Shinyanga na Simiyu), Frank Habibu Mahimbali ameipongeza ofisi ya mashtaka Taifa kwa ubunifu huo wa kujenga ofisi ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga huku akihimiza watumishi wa mashtaka hayo  kufanya kazi kwa kasi zaidi kwa kuwa tayari miundombinu ni rafiki.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude naye amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha haki jinai na utawala bora unapewa nafasi kubwa nchini huku akisema ofisi hiyo itasaidia kuharakisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala katiba na sheria amesema ofisi ya mashtaka itaendelea kupewa kipaumbele katika suala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Sisi watu wa Shinyanga tunayofuraha kubwa sana kuona ujenzi huu wa jengo la Mashtaka umekamilika lakini kwa niaba ya kamati ya kudumu ya Bunge naomba kutoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti kuwa kamati imefurahishwa sana na imevutiwa sana na usimamizi mzuri wa mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Mwakitalu hasa kwenye usimamizi wa fedha za miradi”,amesema.

“Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imejikita kuhakikisha kwamba huduma zinazotolewa na Mahakama zinatolewa katika kiwango bora kwa wakati ili kila mtanzania anufaike na huduma bora ya kisheria ambayo ni matarajio ya kila mtanzania kwamba katika haki inayotolewa na sheria ndiyo msingi wa kujenga amani”, amesema Mhe. Butondo.

“Sisi sote tunafahamu kuwa Bunge linashughulika na kutunga sheria lakini pia hata masula mazima ya kibajeti ya Serikali yetu muhimili wa Mahakama ni muhimili ambao sisi kama wabunge tumekuwa tukitoa kipaumbele kwa kadri ambao bajeti za kwao zinakuja tunawapitishia ili mradi watekeleze miradi yao mbalimbali ya ujenzi wa Mahakama na tunaona huduma zinavyotolewa vizuri kwa wananchi”,amesema.

“Matumaini yetu ya kamati ya Bunge ya utawala katiba na sheria ni kwamba ubora wa jengo hili la mashtaka ni matokeo ya utolewaji wa huduma bora kama matumaini ya watanzania na Bunge kwa ajili ya kutoa huduma bora zilizosahihi za kisheria, sisi tunakuhakikishia katika mahitaji mtakayoyahitaji katika ofisi ya mashtaka tutahakikisha inapewa kipaumbele na hasa katika miradi ya maendeleo”,amesema Mhe. Butondo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Sylivester Mwakitalu akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini , Sylivester Mwakitalu akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa.
Uzinduzi wa Jengo ukiendelea
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Dkt. Khatibu Kazungu na viongozi mbalimbali wakitembelea na kukagua vyumba katika jengo la ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu na viongozi mbalimbali wakitembelea na kukagua vyumba katika jengo la ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu na viongozi mbalimbali wakitembelea na kukagua vyumba katika jengo la ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu na viongozi mbalimbali wakitembelea na kukagua vyumba katika jengo la ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga
Katibu wa Wizara ya Sheria nchini Dotto Henry akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria katika hafla ya ufunguzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga Frank Habibu Mahimbali akizungumza leo kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Naibu meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mawakili Tanganyika, Wakili Sullusi akizungumza
Kamishna wa Huduma za Sheria Veronica Matikila akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Kwaya ya AICT Makongoro kutoka Mwanza ikiimba wimbo maalum katika hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga.
Hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa ikiendelea.
Hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa ikiendelea.
Hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa ikiendelea.
Meneja wa mradi huo Mhandisi Ezrael Masawe akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la ofisi ya mashtaka ya Taifa Mkoa wa Shinyanga.
Hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa ikiendelea.

Hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo jipya la ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya majengo mengine tisa (9) ya ofisi za mashtaka za Mikoa ikiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post