MGODI WA MWADUI, HALMASHAURI YA KISHAPU WASAINI HATI YA MAKUBALIANO UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UWAJIBIKAJI KWA JAMII 'CSR'

Zoezi la utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024 likiendelea

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katika kudhihirisha kuwa uwekezaji katika sekta ya madini unazidi kunufaisha wananchi, Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited (WDL) umesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo kwa mwaka 2023/2024 mgodi huo umetoa kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kufanikisha miradi 16 ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi katika halmashauri hiyo.

Hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imefanyika leo Jumatano Machi 6,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkude amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hali inayopelekea kupatikana kwa fedha na mipango ya kutekeleza miradi ya CSR kwa halmashauri ya wilaya Kishapu huku akiushukuru Mgodi wa Mwadui kwa namna wanavyoshirikiana na halmashauri hiyo kutekeleza miradi ya maendeleo.

Ameupongeza Mgodi wa Mwadui kwa kutoa fedha za CSR, ambazo zitatumika kutekeleza miradi ya kimkakati na kijamii hivyo kusisitiza zitolewe kwa wakati ili miradi itekelezwe kwa wakati.

"Mwaka 2023 Mgodi wa Mwadui ulitoa tena fedha za CSR Sh.bilioni 1.2 ambayo ilitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo,na Mwaka huu wametoa tena Sh.bilioni 1 ambayo itatekeleza Miradi 16 ya Maendeleo. Fedha hizi zinakwenda kutekeleza Miradi ya Maendeleo ambayo inaigusa Jamii, sababu imeibuliwa na wananchi wenyewe," amesema Mkude.

Ameitaja miradi itakayotekelezwa kwa fedha za sehemu ya asilimia 60 (Milioni 600) kuwa ni pamoja na ujenzi wa vizimba 200 katika soko la Kijiji cha Maganzo, ujenzi wa matundu matano ya vyoo katika soko la Kijiji cha Maganzo, ujenzi wa uzio awamu ya kwanza mita 400 katika stendi ya Maganzo, uwekaji taa 8 za solar awamu ya kwanza katika stendi ya Maganzo, uwekaji wa bango la kutambulisha stendi ya Maganzo, kufanya marekebisho ya barabara katika stendi ya Maganzo, kutengeneza madawati 1,346 ya shule za Sekondari na madawati 2,100 ya shule za msingi na usimamizi na ufuatiliajiwa miradi ya CSR.

“Miradi itakayotekelezwa kwa fedha za sehemu ya 40% ni ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Buchambi, ukamilishaji zahanati ya Mpumbula, ukamilishaji wa jengo la OPD kituo cha afya Maganzo, ujenzi wa maabara katika kituo cha afya Maganzo, ujenzi wa matundu matano ya vyoo, Placenter pit na kichomea taka katika kituo cha afya Maganzo, Ujenzi ofisi ya Kijiji cha Songwa, ujenzi wa darasa shule ya msingi Mwangombolwa na kuanzisha ujenzi wa zahanati ya Wizunza”,ameeleza.

Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo amesema mgodi wa Mwadui utaendelea kushirikiana na halmashauri ya Kishapu katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayogusa wananchi.

Mihayo amesema wametekeleza takwa la Kisheria kwa kutoa fedha hizo za CSR Sh.bilioni 1 ikiwa ni asilimia 0.7 ya pato ghafi.

Aidha ameiomba Serikali wakiwemo na viongozi kutoka vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi waimarishe ulinzi na kuzuia uvamizi ndani ya mgodi huo ili wasije kusitisha uzalishaji, bali waendelee na uzalishaji hali ambayo itaongeza mapato ya CSR.

Mihayo amesema licha ya kwamba matukio ya uvamizi katika mgodi yamepungua ameomba halmashauri na jamii kuendelea kushirikiana na mgodi huo kuimarisha ulinzi na usalama katika mgodi huo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. William Jijimya ameushukuru mgodi huo kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya CSR na ushirikiano wanaotoa kwa halmashauri.

Amesema kati ya fedha hizo Sh.bilioni 1, asilimia 60 zitatekeleza miradi ya kimkakati na asilimia 40 zitatekeleza miradi ya maendeleo katika Vijiji 12 ambavyo vinazunguka Mgodi wa Mwadui.

“Tunahitaji amani, tunahitaji kutambua kuwa mgodi huu ni mali yetu, WDL ni ya kwetu na imekuwa ikitusaidia sana, lazima tuulinde mgodi huu”,amesema Jijimya.

Naye Mwenyekiti wa Vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Mwadui, Charles Manyenye na Mwenyekiti wa kata zinazozunguka Mgodi wa Mwadui, Mbalu Lwinzi Kidiga wameupongeza Mgodi huo kwa kuendelea kutoa fedha za CSR ambazo zimeendelea kuimarisha mahusiano mazuri kati ya wananchi na mgodi na kwamba fedha hizo zitasaidia katika kuchochea maendeleo katika jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akizungumza leo Jumatano Machi 6,2024  wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude akizungumza leo Jumatano Machi 6,2024  wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo,
 akizungumza leo Jumatano Machi 6,2024  wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo,
 akizungumza leo Jumatano Machi 6,2024  wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo,
 akizungumza leo Jumatano Machi 6,2024  wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo,
 akizungumza leo Jumatano Machi 6,2024  wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Zoezi la utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024 likiendelea
Zoezi la utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024 likiendelea
Zoezi la utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024 likiendelea
Afisa Uhusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Bernard Mihayo (kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Sabinus Chaula (katikati) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe, William Jijimya wakionesha  Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe, William Jijimya akizungumza leo Jumatano Machi 6,2024  wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mwenyekiti wa Vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Mwadui,  Charles Manyenye akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mwenyekiti wa kata zinazozunguka Mgodi wa Mwadui,  Lwinzi Kidiga akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited uliopo Mwadui kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Sabinus Chaula akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited 
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited 
Diwani wa Kata ya Songwa Mhe. Abdul Ngoromole akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Mmiliki wa Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Limited 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post