MKUU WA MKOA WA SHINYANGA CHRISTINA MNDEME AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA SUKARI... "6 WAMEDAKWA KWA KUPANDISHA BEI'

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akizungumza na Wafanyabiashara wa Sukari Mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekutana na kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara wa Sukari Mkoani Shinyanga ili kujadili namna ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa sukari ambapo sasa bei ya kilo moja inauzwa hadi shilingi 5,000.

Mkutano huo umefanyika leo Jumanne Februari 27,2024 Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa pia na Maafisa Biashara na Wakuu wa Wilaya mkoa wa Shinyanga.

“Tumekutana hapa ili tujadili kuhusu changamoto ya upatikanaji wa sukari. Bei elekezi inayotakiwa ni shilingi 2,600/= hadi 2,800/= kwa bei ya jumla na shilingi 2,800/= hadi 3,000/= kwa bei ya rejareja lakini sasa hivi wananchi wanauziwa hadi shilingi 5,000/= kwa kilo moja ya sukari”,amesema Mndeme.

Amesema katika Mkoa wa Shinyanga kuna tatizo la bei ya Sukari kutokuwa Rafiki wa walaji, hivyo ameona akutane na Wafanyabiashara hao ili kuzungumza nao tatizo nini wameshindwa kuuza Sukari kwa bei elekezi ya Serikali.

Kuna nini kwa wafanyabiashara mnashindwa kuuza Sukari kwa bei elekezi ya Serikali, mnaficha Sukari na kwanini, mpaka tunafikia hatua ya kukamata. Mpaka sasa tumekamata wafanyabiashara sita wa sukari kati watatu ni wafanyabiashara wadogo na watatu ni wafanyabiashara, tumewakamata kwa kwenda kinyume na bei elekezi iliyotolewa na serikali kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Shinyanga. Sasa badala ya kuendelea kukamatana, kuvutana nimeona tuitane hapa ili tujadili kuhusu changamoto hii ya sukari”,ameongeza Mhe. Mndeme.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wamesema kwamba tatizo siyo wao ambao wanasabisha bei ya Sukari kuwa juu, bali ni kwenye Viwanda na maeneo ambayo wanauziwa Sukari hiyo, kuwa bei elekezi ya Serikali haiendani na uhalisia wa bei ya Sokoni ambayo wananunua sukari.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akizungumza na Wafanyabiashara wa Sukari Mkoani Shinyanga leo Februari 27,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akizungumza na Wafanyabiashara wa Sukari Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akizungumza na Wafanyabiashara wa Sukari Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme  akizungumza na Wafanyabiashara wa Sukari Mkoani Shinyanga.
  

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post