WAKULIMA WASHAURIWA KUTOTUMIA MAZAO YALIYOTUMIKA MSIMU ULIOPITA WA KILIMO KAMA MBEGU


Mkaguzi kutoka Taasisi ya Kuthibiti ubora wa mbegu (TOSCI) Nugwa Fortunatus (kushoto) akifafanua jambo kuhusu matumizi ya mbegu bora kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro mbele ya mwezeshaji wa mafunzo hayo Joseph Ngura katika mafunzo yaliyofanyika mjini Morogoro. 
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mafunzo ya matumizi ya mbegu bora yaliyoandaliwa na TOSCI na kufanyika mjini Morpgoro.

 Na Christina Cosmas, Morogoro

WAKULIMA nchini wameaswa kutotumia mazao waliyotumika katika msimu wa kilimo uliopita kama mbegu bali watumie mbegu zilizothibitishwa ubora na zenye lebo ya Taasisi ya kuthibiti ubora wa mbegu nchini (TOSCI) ili kuepukana na changamoto ya kupata mazao kidogo tofauti na matarajio.

Mkaguzi wa mbegu kutoka (TOSCI) Nugwa Fortunatus amesema hayo wakati TOSCI ikitoa mafunzo kwa waandishi wa Habari mkoani Morogoro yaliyofanyika mkoani hapa.

Fortunatus anasema wapo wakulima wanatumia mazao waliyovuna mashambani mwaka uliopita kama mbegu na baadae kuja kulalamikia makampuni ya mbegu wakipata mazao kidogo tofauti na matarajio yao.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Thadei Hafigwa anasema mafunzo kama hayo kwa waandishi wa Habari ni mazuri ambayo humjenga mwanahabari katika kuelimisha wakulima sambamba na kuwa mkulima bora.

Anasema wakulima wanapaswa kutambua kuwa kwa kutumia miongozo, taratibu na sheria za mbegu zilizopo wanaweza kulima na kupata mazao yenye tija.

Akizungumza kwenye kikao hicho Afisa kutoka taasisi inayoshughulika na mifumo ya masoko ya kilimo (AMDT) Joseph Mosha anasema mkulima anapaswa kuhakikisha amenunua mbegu bora zilizothibitishwa na TOSCI zitakazomsaidia kupata mazao bora na kupata mavuno bora bila kupata hasara.

MWISHO….

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments