RAIS SAMIA KUONGOZA MAZISHI YA LOWASSA... HII HAPA RATIBA YA MATUKIO

 Februari 11, 2024

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA KUONGOZA MAZISHI YA LOWASSA FEBR. 17

#Waziri Mkuu atoa ratiba ya matukio.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza Mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa yanayotarajiwa kufanyika Wilayani Monduli Mkoani Arusha Jumamosi Februari 17, 2024.


Awali Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa ambapo bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kuanzia tarehe 10 Februari, 2024. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapilii, Februari 11, 2024) wakati akitoa taarifa ya ratiba ya mazishi ya kiongozi huyo, Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Oysterbay, Dar es Salaam.

Amesema katika kipindi cha siku tano za maombolezo, Taifa litaendelea na shughuli za umma na kijamii sambamba na kushirikiana na wanafamilia katika ratiba ya msiba kama ilivyoandaliwa na kamati ya mazishi ya Kitaifa na wanafamilia.

Amesema kabla ya mazishi hayo mwili wa Hayati Lowassa unatarajiwa kuagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


Amesema Jumanne Februari 13, 2024 mwili wa Hayati Lowasa unatarajiwa kuagwa na viongozi na wananchi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Jumatano Februari 14 mwili wa Hayari Lowasa  utapelekwa katika Kanisa la KKKT Azania Front kwa ajili ya ibada takatifu na kuaga.


Amesema Alhamisi Februari 15 mwili wa Hayati Lowassa utasafirishwa hadi jijini Arusha ambapo viongozi na wananchi watapa fursa ya kuaga katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.


Waziri Mkuu huyo mstaafu alifariki jana (Jumamosi, Februari 10, 2024) wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam na tangazo la kifo chake lilitolewa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, FEBRUARI 11, 2023.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post