MSAFARA WA MAKONDA WAPATA AJALI, MAGARI 10


Msafara wa Katibu wa NEC Itikadi ,Uenezi na Mafunzo wa CCM Paul Makonda umepata ajali katika eneo la Masasi mkoani Mtwara.

Ajali hiyo iliyotokea leo Jumapili  saa 9 alasiri imehusisha magari 10 yaliyokuwepo katika msafara wa muenezi Makonda uliokuwa unatoka mkoani Ruvuma kuelekea jijini Dar es salaam

Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu wawili wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mtwara na huku kukiwa hakuna kifo chochote.

Hata hivyo kwa upande wa hali ya kiafya ya katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Paul Makonda ipo salama.


Chanzo - Wasafitv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post