DKT. BITEKO AWASILI KENYA KUHUDHURIA MKUTANO WA EAPP

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Kenya kuhudhuria Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wanaohusika na mfumo wa pamoja wa umeme kwa nchi za Mashariki ya Afrika (EAPP Council of  Ministers) utakaofanyika tarehe 27 na 28 Februari, 2024 jijini Nairobi.

Katika Ziara hiyo Dkt. Dotto Biteko ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Wakili Stephen Byabato(Mb), na kupokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Benard Kibesse akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati wa Kenya, Mhe. Alex Wachira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post