NAIBU KATIBU MKUU WA AFYA DKT. GRACE MAGEMBE AKAGUA HUDUMA NA MIRADI YA AFYA SHINYANGA, ATAKA MAADILI KWA WATUMISHI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amefanya ziara mkoani Shinyanga ambapo ametembelea Kituo cha Afya Kambarage kujionea namna huduma za afya zinavyotolewa, pia amekagua huduma zinazotolewa katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura na ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Katika ziara hiyo ya kukagua huduma na miradi ya afya aliyoifanya leo Ijumaa Februari 23,2024 Dkt. Magembe pia amekagua miradi ya ujenzi na utoaji huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

PICHA na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (katikati aliyesimama) akiangalia kwenye mtandao huduma zinazotolewa katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde & Marco Maduhu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (katikati aliyesimama) akiangalia kwenye mtandao huduma zinazotolewa katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembea akitembelea Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (katikati) akikagua ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia) akikagua ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia) akikagua ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Robert Elisha akimwelezea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe kuhusu ujenzi unaoendelea wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia) akisalimiana na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Robert Elisha baada ya kuwasili katika Kituo cha Afya Kambarage
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (katikati) akisalimiana na wananchi waliofika kupata huduma za afya katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Mmoja wa wananchi akimwelezea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe kuhusu huduma za afya katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na wananchi katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na wananchi katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia katikati) akiwa katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (kulia katikati) akiwa katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga.
.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Grace Magembe akifuatilia huduma za mapokezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Grace Magembe akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiangalia namna uzalishaji wa Hewa ya Oxgyen katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.

Habari na Marco Maduhu, SHINYANGA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amefanya ziara mkoani Shinyanga na kutoa maagizo kwa Watumishi wa Afya kutoa huduma stahiki za matibabu kwa wagonjwa.

Amefanya ziara hiyo leo Februari 23,2024, kwa kuona utoaji wa huduma za Afya katika Kituo cha Afya Kambarage, huduma za jengo la wagonjwa wa dharura na Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje  Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na huduma za matibabu hospitali ya Rufaa Mkoa pamoja na kuzungumza na watumishi wa Afya.

Amesema Serikali imeboresha utoaji wa huduma za matibabu kwa wananchi kwa kujenga Zahanati,Vituo vya Afya, hospitali pamoja na kutoa vifaa tiba vya kisasa, na hivyo kuwataka Watumishi wa Afya kutoa huduma stahiki za matibabu kwa wagonjwa.

Amesema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Serikali itaongeza pia ujenzi wa Majengo matano ili kuboresha huduma za Matibabu, ikiwemo ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto,Maabara, Stoo ya dawa, Mochwari na Jengo la kufua nguo za Wagonjwa.

"Tunataka Maboresho haya ya huduma za Afya, yaendane na utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wananchi," amesema Dkt. Magembe.

Katika hatua nyingine ametoa Maagizo kwa Watumishi wa Afya, kuzingatia Miiko,Sheria,kanuni na maadili ya taaluma zao pamoja na kutunza siri za wagonjwa.

Amesema kwa Mtumishi wa Afya ambaye anakwenda kinyume na maadili ya Taaluma yake na kuitia doa Sekta hiyo, hawatasita kumchukulia hatua kwa kumuondoa kazini na hata kumfutia Leseni yake.

Pia ameagiza ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga,kwamba ukamilike kwa wakati ili lianze kutumika kutoa huduma kwa wananchi, ambalo linatarajiwa kukamilika Machi mwaka huu.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile, ameipongeza Serikali kwa kuboresha huduma za Afya mkoani humo,na kwamba baadhi ya huduma ambazo wananchi walikuwa wakienda kupata Hospitali ya Rufaa Bugando Jijijini Mwanza,sasa hivi zinapatikana mkoani humo.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, amesema maelekezo yote ambayo yametolewa watayafanyia kazi, ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post