MAAFISA ELIMU WATOA MIL.20/- KWA WAATHIRIKA WA MAAFA YA HANANG


OR- TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amekabidhi Sh.Milioni 20 kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama kutoka kwa  Umoja wa Maafisa Elimu wa Mkoa na Halmashauri zote nchini kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Hanang mkoani Manyara.

Mhe. Mchengerwa amekabidhi fedha hizo leo (09 Januari, 2024) kwa Waziri Jenista katika Ofisi yake ndogo Jijini Dar es salaam, ambapo amepokea fedha hizo kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mchengerwa amesema fedha hizo zilitolewa kwenye Mkutano wa Maafisa Elimu hao mwishoni uliofanyika Manispaa ya Morogoro ambapo Maafisa hao  wametoa mchango wao kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwahudumia wananchi wa Hanang waliopatwa  na maafa ya maporomoko ya mawe na tope.

"Maafisa Elimu kwa ushirikiano wao waliona umuhimu wa kuchangishana na kusaidia waathirika wa maafa yaliyotokea Hanang na kunituma nikukabidhi wewe Mhe.Waziri mwenye dhamana,"amesema.

Naye, Waziri Mhagama amewashukuru kwa mchango huo na kuunga mkono serikali katika kuhudumia wananchi hao na kwamba fedha hizo zimewekwa kwenye Akaunti ya maalum ya maafa iliyoko Benki Kuu.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post