WABUNGE PATROBAS KATAMBI , SANTIEL KIRUMBA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA WAFUNGWA SHINYANGA

 


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba, wametoa Ng’ombe wa Krismasi Magereza ya wilaya ya Shinyanga.

Ng’ombe huyo amekabidhiwa leo Decemba 24, 2023 na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson kwa niaba ya Wabunge hao, kwa Mkuu wa Magereza ya wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi, pamoja na Shilingi Laki 2 iliyotolewa na Mbunge Katambi kwa ajili ya kununua Sabuni za kufulia.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Ng’ombe na fedha Sh.Laki 2, Samwel amesema Mbunge Katambi na Santiel, waliahidi kutoa Ng’ombe kwenye Magereza ya wilaya ya Shinyanga, na leo wametekeleza ahadi yao ili askari Magereza pamoja na wafungwa washerehekee Siku Kuu ya Krismasi kwa furaha na upendo.

“Mbunge Katambi pamoja na Santiel waliahidi kutoa Ng’ombe wa Krismasi katika Magereza hii ya wilaya ya Shinyanga, na wametekeleza ahadi yao na thamani ya Ng’ombe huyu ni Sh, Laki 7, nimekabidhi pia na Sh.Laki 2 ambazo zimetolewa na Mheshimiwa Katambi kwa ajili ya kununua sabuni za kufulia ni moja pia ya ahadi yake kwa wafungwa,”amesema Samweli.
“Mheshimiwa Katambi na Santiel wanawatakia Askari Magereza na wafungwa wote, heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2024,”ameongeza Samweli.

Naye Mkuu wa Magereza ya wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi, amewashukuru Wabunge hao kwa zawadi hiyo waliowapatia ya Ng’ombe kwa ajili ya Siku Kuu ya Krismasi na kutekeleza ahadi yao, pamoja na fedha Sh.Laki 2 ya kununua Sabuni za kufulia nguo za wafungwa, na kutoa wito pia kwa viongozi wengine wawe wanawakumbuka na wafungwa katika Sherehe mbalimbali.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson (kushoto) akikabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga aliyetolewa na Wabunge Katambi na Santiel Kirumba, (kulia)ni Mkuu wa Magereza hiyo Theophil Mulokozi.
Zoezi la kukabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Zoezi la kukabidhi Ng'ombe wa Christimas katika Magereza ya wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samwil Jacskon (kushoto)akibidhi Sh. Laki 2 kwa Mkuu wa Magereza wilaya ya Shinyanga Theophil Mulokozi pesa iliyotolewa na Mbunge Katambi kwa ajili ya kununua Sabuni za kufulia.
Picha ya pamoja ikipigwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post