CCM YATOA SALAMU KWA VIONGOZI VIJANA WANAWAKE KUTOKA NCHI 16 ZA AFRIKA

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Anamringi Macha akizungumza wakati wa kutoa salaam za CCM, Jumanne, Disemba 12, 2023, kwa viongozi vijana wanawake kutoka nchi 16 za Afrika wanaohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Asasi ya Kiraia ya Young Women of Africa (YWOA), wanaotoka katika vyama tawala katika nchi hizo.

 Mkutano huo unaoendelea katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, iliyoko Kibaha, mkoani Pwani, unafanyika sambamba na mafunzo na mijadala ya masuala anuai yanayowahusu wanawake na uongozi katika nyanja mbalimbali kwenye jamii za Afrika na dunia kwa ujumla na kuweka maazimio yatayakochangia mstakabali wa jamii zilizo bora zaidi kwa kila mmoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post