MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI DODOMA....AONYA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo tarehe 10 Desemba 2023.Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Makamu wa Rais amewaasa watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii.


Amesema matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema pamoja na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais amewashukuru waumini hao kwa kuendelea kumuombea ili aweze kutekeleza vema majukumu yake.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post