KIKUNDI CHA NGUVU MOJA SHINYANGA KUJA NA MIPANGO MADHUBUTI YA KUINUANA KIUCHUMI


Kikundi cha Nguvu Moja kilichopo manispa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga kimeshauriwa kuja na mipango madhubuti ya uanzishaji wa miradi itakayosaidia jamii pamoja na wanachama wa kikundi hicho.

Ameyasema hayo jana Novemba 18,2023 afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale wakati akizungumza na wanachama wa kikundi cha Nguvu Moja kwenye hafla ya kuanzishwa kwa kikundi hicho.

Amesema ni wakati sasa wa vikundi na wanachama kufikiri kwa mapana zaidi namna ya uanzishaji wa miradi kwenye vikundi vya kusaidiana, itakayowasaidia wanachama na jamii kwa ujumla.

“Tusiishie tu kusaidiana kwenye shida na raha bali tuangalie namna gani tunaweza kuisaidia jamii, na kuwa mfano kwa vikundi vingine, vikundi vingi vinavyoanzishwa vinashindwa kuendelea kutokana na kushindwa kubuni na kusimamia miradi itakayowainua wanachama, mbali na kusaidiana katika shida na raha, tuangalie pia namna gani tunaweza kuisaidia jamii kupitia vikundi tunavyovianzisha", 

"Kupitia fursa zilizopo ndani ya mkoa huu, twendeni tukazalishe kwa ukubwa ili tuweze kuleta manufaa kwa wanakikundi na jamii inayowazunguka, na hatimaye malengo ya kiukundi hiki yakaonekane ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga, macho hayana thamani ikiwa mawazo yetu yamefungwa”, aliongeza Tedson Ngwale.

 Akisoma risala kwa mgeni rasmi Velma Moris ameeleza malengo ya kikundi hicho ikiwa ni pamoja na kusaidiana baina ya wanachama katika shida na raha sambamba na kutoa mafunzo ya biashara na ujasiriamali ili kutengeneza jamii yenye kusimamia uchapaji kazi.

“Kikundi hiki kilianzishwa tarehe 20/11/2022 kikiwa na wanachama 20 kwa lengo la kukuleta umoja  baina ya wanachama ili kusaidiana katika shida na raha ambapo kwa sasa kina wanachama 53, ambapo 45 ni wanawake na 8 ni wanaume, tumejipanga kuanzisha miradi mbalimbali itakayoweza kuendesha kikundi chetu, lakini pia tumedhamiria kwa siku zijazo kutoa mafunzo kwa wanachama juu ya ujasiriamali na biashara kwa wnanchama ili kusaidia wanachama kupata ujuzi wa kukuza na kuendesha biashara, lakini pia kuwa mabalozi wa kupinga vitendo vya ukatili,” alisema Velma Moris.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi , afisa tarafa ya Samuye Aaron Laizer amekipongeza kikundi hicho kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake  huku akimuomba afisa maendeleo mkoa kutoa elimu kwa wanachama na vikundi mbalimbali ili kuwajengea uwezo.

“Niwapongeze sana kwa idadi kubwa ya wanawake kwenye kikundi hiki cha nguvu moja hii ni wazi kuwa mmetambua nafasi ya mwanamke kwa kutoa kipaumbele, pia kwa hotuba hii kutoka kwa mgeni rasmi nilitamani ikawe mafunzo kwa wananchama na vikundi mbalimbali kuwajengea uwezo waweze kuwa na mawazo nyenye kuleta mafanikio makubwa”, Alisema Aaron Laizer.

 Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza na wanachama wa kikundi cha Nguvu Moja.

Velma Moris  akisoma risala ya kikundi cha Nguvu Moja wakati wa hafla  hiyo.

 Afisa tarafa ya Samuye Aaron Laizer akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi wakati wa Hafla hiyo.

Wanachama wa kikundi cha Nguvu Moja.

Mwenyekiti wa kikundi cha Nguvu Moja Leopodin Masai akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Katibu wa kikundi cha Nguvu Moja Kosta Kasisi Akizungumza wakati wa hafla hiyo.

<<<<PICHA MBALIMBALI>>>>






















 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post