JAJI MWANGESI : JUKUMU LA BARAZA LA MAADILI NI KUUDHIHIRISHIA UMMA KUWA HAKI NI UKWELI UNAOPATIKANA KWA KILA MTU




Katibu Ukuzaji Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Kipacha,akifungua mafunzo kwa wajumbe wa Baraza la Maadili (hawako pichani) leo Novemba,6, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Point Zone Resort jijini Arusha.


Picha ya pamoja kati ya Mhe. Jaji (Mst.) Rose Teemba, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili (katikati), Bibi. Suzan Mlawi, Mjumbe wa Baraza la Maadili (kulia kwa Mwenyekiti), Bw. Waziri Kipacha, Katibu Ukuzaji Maadili na baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wajumbe wa Baraza la Maadili yaliyofanyika tarehe 6 Novemba, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Point Zone Resort jijini Arusha.

................

Mhe. Jaji (Mst.) Sivangilwa Mwangesi amesema kuwa wajumbe wa Baraza la Maadili wana jukumu la kusimamia haki na kuudhihirishia umma kuwa haki siyo dhana, bali ni ukweli unaopatikana kwa kila mhusika.

Amesema hayo tarehe 6 Novemba, 2023 katika ukumbi wa hoteli ya Point Zone Resort jijini Arusha wakati wa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa wajumbe wa Baraza la Maadili iliyosomwa kwa niaba yake na Bw. Waziri Kipacha, Katibu Ukuzaji wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma.

“Kama wajumbe wa Baraza la Maadili nyinyi ni kiunganishi baina ya Sheria na watu wanaolengwa kusaidiwa na Sheria. Mnatakiwa kuuhakikishia umma kwamba haki siyo dhana bali ni ukweli unaopatikana kwa kila muhusika,” amesema.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Maadili, jukumu la Wajumbe wa Baraza la Maadili ni muhimu katika eneo la uadilifu wa Vingozi wa Umma kwasababu wao ndio husimamia haki, kuhakikisha usawa na kuimarisha Utawala Bora ndani ya jamii yetu.

“Jukumu lenu linachukuliwa kwa uzito mkubwa ndio sababu tuko hapa. Mnabeba jukumu kubwa linalogusa maisha ya wananchi kwa mahusiano yao na Serikali yao. Mnayofanya yanatoa muelekeo wa haki na kazi yenu inaathiri maisha ya watu wanaokuja mbele ya Sekretarieti ya Maadili kutafuta haki na ufumbuzi wa malalamiko yao kuhusiana na Viongozi wa Umma,” amesema.

Aidha, wajumbe hao wa Baraza la Maadili, katika kipindi hiki cha mafunzo yanayohusu utekelezaji wa majukumu yao, watapitishwa katika mada mbalimbali ikia ni pamoja na utambuzi wa makosa ya kimaadili, namna ya kushughulikia mashauri yanayowasiishwa mbele ya Baraza na kupata uzoefu kutoka mataifa mengine duniani.

Mafunzo hayo yanafanyika chini ya ufadhili wa Program endelevu ya kujenga uwezo kwa Taasisi katika kupambana na rushwa nchini Tanzania (Building Sustainable Ant corruption Action in Tanzania BSAAT).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post